AMISOM yakanusha madai ya Al Shabab kuuteka mji wa kistratijia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53152-amisom_yakanusha_madai_ya_al_shabab_kuuteka_mji_wa_kistratijia
Kikosi cha Kijeshi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kimekanusha habari kuwa kundi la kigaidi la al-Shabab limetwaa tena mji wa Sabiid kwenye wilaya ya kusini uliokombolewa hivi karibuni.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 28, 2019 23:39 UTC
  • AMISOM yakanusha madai ya Al Shabab kuuteka mji wa kistratijia

Kikosi cha Kijeshi cha Umoja wa Afrika nchini Somalia (AMISOM) kimekanusha habari kuwa kundi la kigaidi la al-Shabab limetwaa tena mji wa Sabiid kwenye wilaya ya kusini uliokombolewa hivi karibuni.

AMISOM imethibitisha kuwa mji wa Sabiid bado unadhibitiwa na Jeshi la Serikali ya Somalia linaloungwa mkono na AMISOM. Mjio huo muhimu kistratijia uko umbali wa kilomita 40 kusini mwa mji mkuu Mogadishu

AMISOM imesema vikosi vya ushirikiano vitaendelea kusimamia amani nchini Somalia, na kupuuza habari kuhusu kuchukuliwa kwa mji wa Sabiid kama propaganda za al-Shabab.

Umoja wa Mataifa unafadhili askari hao wa Amisom ambao sasa ni 21,000 na wamekuweko nchini Somalia tokea mwaka 2007. Wanajeshi wa Amisom walioko Somalia ni kutoka Uganda, Kenya, Burundi, Somalia, Ethiopia, Djibouti na Sierra Leone. Nao maafisa wa polisi wa AMISOM ni kutoka Nigeria, Sierra Leone na Uganda.