Ujumbe wa Siku ya Wafanyakazi (Mei Mosi) nchini Kenya + Sauti
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53213-ujumbe_wa_siku_ya_wafanyakazi_(mei_mosi)_nchini_kenya_sauti
Jamii ya wafanyakazi nchini Kenya imeitaka serikali kumaliza tatizo la ufisadi ambalo limeshika kasi sana nchini. Hayo yametolewa na wafanyakazi hao katika sherehe za Siku ya Mfanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo pamoja na mambo mengine wameitaka serikali ya Nairobi kuwaandalia mazingira salama ya kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 01, 2019 11:28 UTC

Jamii ya wafanyakazi nchini Kenya imeitaka serikali kumaliza tatizo la ufisadi ambalo limeshika kasi sana nchini. Hayo yametolewa na wafanyakazi hao katika sherehe za Siku ya Mfanyakazi Duniani Mei Mosi ambapo pamoja na mambo mengine wameitaka serikali ya Nairobi kuwaandalia mazingira salama ya kazi ili waweze kutekeleza majukumu yao ipasavyo.

Aidha wameikosoa serikali ya Kenya kwa kuendelea kukopa fedha kiholela nje ya nchi na kwamba hatua hiyo imeifanya serikali hiyo kupandisha kodi katika sekta mbalimbali dhidi ya wananchi ikiwa ni katika juhudi za kulipa madeni hayo. Hii ni katika hali hali ambayo serikali imegoma kutangaza nyongeza ya mishahara kwa asilimia yoyote ile, suala ambalo linatoa ujumbe kwa wafanyakazi kwamba sasa wanatakiwa kukaza Kamba, ili kuweza kumudu gharama za maisha.

Kwa maelezo zaidi tujiunge na mwandishi wetu wa jijini Mombasa, Seifulla Murtadha………/