51 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila katikati mwa Kodivaa
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i53549-51_wauawa_na_kujeruhiwa_katika_mapigano_ya_kikabila_katikati_mwa_kodivaa
Polisi ya Kodivaa (Ivory Coast) imeripoti kuwa watu 51 wameuawa na kujeruhiwa katikamapigano ya kikabila katikati mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
May 17, 2019 13:36 UTC
  • 51 wauawa na kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila katikati mwa Kodivaa

Polisi ya Kodivaa (Ivory Coast) imeripoti kuwa watu 51 wameuawa na kujeruhiwa katikamapigano ya kikabila katikati mwa nchi hiyo.

Kwa mujibu wa polisi ya Kodivaa, hadi sasa watu saba wameaga dunia na wengine 44 kujeruhiwa katika mapigano ya kikabila yaliyojiri katika mji wa Beoumi katikati mwa nchi hiyo kuanzia juzi Jumatano. Awali Djedj Mel Kamishna wa polisi wa mji wa beoumi palipojiri mapigano hayo alisema kuwa watu watatu wameuawa na 40 kujeruhiwa katika mapigano yaliyojiri katika mji huo.  

Kamishna huyo wa polisi  ameongeza kuwa tayari wamechukua hatua na kutangaza marufuku ya kutotembea kuanzia saa kumi na mbili jioni hadi asubuhi. Mapigano ya kikabila yameshtadi huko Kodivaa katika miezi kadhaa ya karibuni.