Magaidi 100 wangamizwa katika mkoa wa Hama nchini Syria
(last modified Tue, 28 May 2019 07:54:00 GMT )
May 28, 2019 07:54 UTC
  • Magaidi 100 wangamizwa katika mkoa wa Hama nchini Syria

Kituo cha Upatanishi cha Russia nchini Syria kimesema kuwa, jeshi la nchi hiyo limevunja shambulizi la magaidi wa Jabhat al Nusra kaskazini mwa mkoa wa Hama na kuangamiza magaidi wasiopungua 100 walioshambulia vituo vya jeshi hilo.

Shirika la habari la Mehr limeripoti leo kuwa, kituo hicho cha upatanishi cha Russia nchini Syria kimesema katika ripoti yake kuwa, magaidi wasiopungua 450 walikuwa wamevamia eneo la Kafr Nabudah la kaskazini mwa mkoa wa Hama katika juhudi za kujaribu kuteka maeneo ya jeshi la Syria, lakini uvamizi huo umefeli.

Kwa mujibu wa ripoti hiyo, wanajeshi wa Syria wamefanikiwa pia kuteketeza vifaru vitatu, vifaa viwili vya kurushia makombora ya aina mbalimbali na gari moja la deraya la magaidi hao.

Wanajeshi wa Syria

 

 

Tarehe 8 Mei 2019, jeshi la Syria lilifanikiwa kuwafurusha magaidi katika eneo la Kafr Nabudah katika viunga vya mkoa wa Hama.

Tangu mwanzoni mwa mwezi huu wa Mei, mkoa wa Idlib na viunga vya kaskazini magharibi mwa mkoa wa Hama vimekuwa vikishuhudia mapigano baina ya jeshi la Syria na magenge ya kigaidi yanayoungwa mkono na Marekani, Israel na Saudi Arabia na maadui wengine wa Syria.

Katika kipindi hicho, jeshi la Syria limepata mafanikio makubwa ikiwa ni pamoja na kuangamiza magaidi wengi na kukomboa ardhi zilizokukwa zimetekwa na kukaliwa kwa mabavu na magaidi hao.

Tags