OCHA: Hali ya kibinadamu ni mbaya kaskazini mashariki mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55135-ocha_hali_ya_kibinadamu_ni_mbaya_kaskazini_mashariki_mwa_nigeria
Umoja wa Mataifa na maafisa wa mashirika ya utoaji misaada wanasema kuwa, hali ya kibinadamu kaskazini mashariki mwa Nigeria ni mbaya ikiwa ni miaka 10 tangu kuzuka machafuko katika maeneo hayo.
(last modified 2026-02-05T09:20:29+00:00 )
Aug 02, 2019 02:48 UTC
  • OCHA: Hali ya kibinadamu ni mbaya kaskazini mashariki mwa Nigeria

Umoja wa Mataifa na maafisa wa mashirika ya utoaji misaada wanasema kuwa, hali ya kibinadamu kaskazini mashariki mwa Nigeria ni mbaya ikiwa ni miaka 10 tangu kuzuka machafuko katika maeneo hayo.

Umoja wa Mataifa na wadau wengine wa misaada wanasema kwamba, mahitaji ya kibinadamu yanaendelea kuongezeka katika maeneo hayo na kwamba, kuyatimiza mahitaji hayo ni changamoto kubwa.

Wadau hao wa masuala ya kibinadamu ukiwemo Umoja wa Mataifa, mashirika yasiyo ya kiserikali, wawakilishi wa serikali, shirika la kitaifa la masuala ya dharura NEMA , na mashirika mengine ya misaada ya kibinadamu walikutana jana katika kumbukumbu ya miaka 10 tangu kuanza kwa machafuko kaskazini mashariki mwa Nigeria na vilevile kuwakumbuka mamilioni ya watu walioathirika na machafuko hayo.

Wakimbizi nchini Nigeria

Katika kumbukumbu hiyo Shirika la Umoja wa Mataifa la kuratibu masuala ya kibinadamu OCHA limesisitiza kuhusu mahitaji makubwa ya kibinadamu yaliyopo kaskazini mashariki mwa Nigeria na ulazima wa kuendelea kuongezwa msaada wa kibinadamu kwa mamilioni ya watu hasa kwenye majimbo matatu yaliyoathirika zaidi na mashambuulio ya kuundi la Boko Haram ya Borno, Adamawa na Yobe.

Kundi la kigaidi la Boko Haram lilibeba silaha na kuanzisha uasi mwaka 2009 kwa lengo la kuasisi utawala eti wa Kiislamu kaskazini mwa Nigeria, ambapo mbali na ndani ya nchi hiyo, limepanua wigo wa mashambulio yake katika nchi jirani pia za Niger, Chad na Cameroon.