Hamas: Israel inawalenga kwa silaha waandishi habari ili kuficha ukweli
(last modified Sat, 03 Aug 2019 08:10:23 GMT )
Aug 03, 2019 08:10 UTC
  • Hamas: Israel inawalenga kwa silaha waandishi habari ili kuficha ukweli

Harakati ya Mapambano ya Kiislamu ya Palestina (Hamas) imekitaja kitendo cha wanajeshi wa utawala wa Kizayuni wa Israel cha kuwafyatulia risasi waandishi habari wanaoripoti maandamano makubwa ya Wapalestina ya Haki ya Kureja katika mipaka ya Ghaza kuwa ni juhudi zilizofel za kutaka kuficha ukweli na jinai za utawala huo.

Msemaji wa Hamas Hazem Qassim amesema kuwa Wazayuni wanakiuka na kupuuza sheria na maazimio ya kimataifa kuhusu haki za kibinadamu kwa kufanya jinai kama hizo. Qassim ametaka kufikishwa mbele ya vyombo vya sheria na kuhukumiwa viongozi wa utawala wa Kizayuni.

Jana Ijumaa waandishi habari wawili walijeruhiwa kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel wakiripoti habari za maandamano ya amani ya Wapalestina  kwenye mipaka ya Ukanda wa Ghaza. 

Hazem Qassim, Msemaji wa Harakati ya Hamas ya Palestina
 

Waandishi habari wengine wawili wa Kipalestina wameuliwa shahidi kwa kupigwa risasi na wanajeshi wa Israel tangu kuanza maandamano ya Haki ya Kurejea Machi 30 mwaka jana na makumi ya wengine mejeruhiwa.  

Tags