Watu wasiopungua 19 waaga dunia Cairo Misri kufuatia mlipuko uliosababishwa na ajali
Wizara ya Afya ya Misri imetangaza kuwa, kwa akali watu 19 wameuawa mapema leo na makumi ya wengine kujeruhiwa baada ya kutokea mripuko nje ya Taasisi ya Taifa ya Saratani katikati mwa mji mkuu wa Cairo.
Taarifa za awali zinasema kuwa, gari moja liligongana na magari mengine matatu na kusababisha mripuko huo. Taarifa zaidi zinasema kuwa, gari hilo lilikuwa likiendeshwa katika barabara moja kinyume na magari mengine yanavyokwenda.
Kwa mujibu wa duru za usalama za Misri, kufuatia ajali hjiyo, kulitokea mlipuko mkubwa ulisababisha kutokea moto mkubwa.
Kiongozi wa Mashtaka wa Serikali ya Misri ameaziambia duru za habari kwamba, anachunguza chanzo cha tukio hilo.
Ingawa hadi sasa hakujatolewa taarifa rasmi lakini baadhi ya duru zisizo rasmi zinasema kuwa, huenda tukio hilo ilikuwa ni shambulio la kupanga.
Majengo ya taasisi hiyo ya maradhi ya saratani yameathirika vibaya na mlipuko huo.
Wizara ya Mambo ya Ndani ya Misri imetangaza kuwa, wagonjwa wote waliokuwako katika kituo hicho cha tiba wamehamishwa