Jamii ya Kimataifa yataka uchaguzi Jubaland, Somalia uwe wa Amani
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55442-jamii_ya_kimataifa_yataka_uchaguzi_jubaland_somalia_uwe_wa_amani
Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zimetoa wito wa kufanyika uchaguzi wa amani na wa haki huko Jubaland, Kusini mwa Somalia, wakisema uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 24 ni muhimu kwa utulivu katika nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 17, 2019 21:53 UTC
  • Jamii ya Kimataifa yataka uchaguzi Jubaland, Somalia uwe wa Amani

Umoja wa Afrika na Umoja wa Mataifa zimetoa wito wa kufanyika uchaguzi wa amani na wa haki huko Jubaland, Kusini mwa Somalia, wakisema uchaguzi uliopangwa kufanyika Agosti 24 ni muhimu kwa utulivu katika nchi hiyo.

Wawakilishi waandamizi kutoka Umoja wa Afrika, Shirika la Maendeleo ya Kiserikali la Nchi za Afrika Mashariki (IGAD) na Umoja wa Mataifa, wamesisitiza haja ya kuwepo kwa mchakato mmoja wa uchaguzi ulioafikiwa ambao utakuwa kwa mujibu wa katiba ya Jubaland na katiba ya serikali ya muda. Kwenye taarifa yao ya pamoja wawakilishi hao wamezitaka pande zote kujiepusha na vitendo vyovyote vya vurugu au vitisho.

Askari wa Umoja wa Afrika wanaolinda amani Somalia

Rais wa sasa Ahmed Madobe anatetea kiti chake lakini anakabiliwa na ushindani mkali kutoka kwa wagombea wengine sita, baadhi yao wakiungwa mkono na serikali ya taifa yenye makao yake Mogadishu.

Mfumo wa utawala Somalia ni wa kifiderali ambapo majimbo kadhaa nchini humo yana mamlaka ya ndani ya kujitawala.