UN yaeleza wasiwasi wake kuhusu mgogoro wa kibinadamu Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i55539-un_yaeleza_wasiwasi_wake_kuhusu_mgogoro_wa_kibinadamu_somalia
Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Somalia ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na ongezeko la mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo na Kiafrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Aug 22, 2019 21:58 UTC
  • UN yaeleza wasiwasi wake kuhusu mgogoro wa kibinadamu Somalia

Mjumbe maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Somalia ameeleza wasiwasi wake kuhusiana na ongezeko la mgogoro wa kibinadamu katika nchi hiyo na Kiafrika.

James Swan amekiambia kikao cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwamba, karibu Wasomali milioni mbili na laki mbili wanasumbuliwa na ukosefu mkubwa wa chakula. 

James Swan ameongeza kuwa, Wasomali wengine wanaokaribia milioni mbili na laki sita wamelazimika kuwa wakimbizi ndani ya nchi kutokana na vita na ukame. 

Afisa huyo wa Umoja wa Mataifa amesema jumuiya hiyo ya kimataiifa ikishirikiana na serikali ya Somalia imetayarisha mpango wa kukabiliana na ukame ambao unahitajia dola milioni 686 na kwamba hadi sasa zimepatikana dola milioni 350 tu kwa ajili ya kutekeleza mpango huo. Swan amezitaka nchi wanachama wa UN kufadhili mpango huo. 

Njaa na mapigano ya ndani vimewalazimisha mamilioni ya Wasomali kuwa wakimbizi

Maafisa wa Umoja wa Mataifa wanasema kuwa, zinahitajika dola bilioni moja na milioni 80 kwa ajili ya kukabiliana na mgogoro wa kibinadamu nchini Somalia katika mwaka huu wa 2019. 

Mwaka 2011 nchi za Pembe ya Afrika ikiwemo Somalia, zilikumbwa na njaa na ukame mkubwa vilivyoambatana na mapigano ya ndani. Nchi za eneo hilo pia zinasumbuliwa na ukosefu wa usalama unaosababishwa na mashambulizi ya mara kwa mara ya wapiganaji wa kundi la kigaidi la al Shabab.