Watu zaidi ya 50 watekwa nyara kaskazini magharibi mwa Nigeria
Watu wasiojulikana wamewateka nyara raia wasiopungua 50 katika shambulizi walilolifanya kaskazini magharibi mwa Nigeria.
Mmoja wa raia ambaye mabinti wake wawili wametekwa nyara amesema kuwa majambazi zaidi ya 100 walikivamia kijiji chao na kufyatua risasi kwa karibu masaa mawili. Hata hivyo hakuna mtu yoyote aliyeweza kupambana na wavamizi hao. Wavamizi hao wasiojulikana wametaka kulipwa pesa ili kuwaachia huru mateka hao.
Eneo la kaskazini magharibi mwa Nigeria ni miongoni mwa maeneo yaliyoathiriwa na machafuko na serikali inaamini kuwa majambazi ndio chanzo cha ukosefu wa amani katika eneo hilo.
Wananchi wa Nigeria wanaamini kuwa kushindwa serikali ya Abuja kuwadhaminia usalama kunapelekea kuongezeka mashambulizi ya kundi la kigaidi la Boko Haram na majambazi na ndio maana eneo la kaskazini magharibi limekuwa likishuhudia machafuko na vitendo vya uhalifu mara kwa mara.