AU: Utamaduni wa kusoma uimarishwe katika nchi za Afrika
(last modified Sun, 22 Sep 2019 07:34:47 GMT )
Sep 22, 2019 07:34 UTC
  • AU: Utamaduni wa kusoma uimarishwe katika nchi za Afrika

Umoja wa Afrika umetoa mwito wa kufanywa kampeni ya kuhimiza utamaduni wa kusoma miongoni mwa vijana katika nchi za Afrika.

Mwito huo umetolewa na Mesfin Tessema, Mkurugenzi wa Taasisi ya Stratejia, Sera, Tathmini na Ukusanyaji wa Rasimali ya umoja huo (SPPMERM) katika kongamano la kieneo linaloendelea katika makao makuu ya AU yaliyoko katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa.

Amesema, "Elimu inaanza na kumalizika kwa kusoma. Watoto wanapaswa kufunzwa wakiwa wadogo kuwa kusoma ni katika ngazi nne muhimu za kukwea katika elimu."

Wanafunzi wakiwa shuleni nchini Burundi

Afisa huyo amenukuu takwimu za AU zinazoonyesha kuwa, bara la Afrika lina kiwango kikubwa cha watu wasiojua kusoma na kuandika ikilinganishwa na maeneo mengine ya dunia.

Kwa mujibu wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Elimu, Sayansi na Utamaduni (UNESCO), kuna watu zaidi ya milioni 750 ambao ni wajinga wa kutojua kusoma na kuandika kote ulimwenguni.