Ufichaji mambo wa serikali ya Nigeria kuhusiana na hali ya Sheikh Zakzaky
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i56897-ufichaji_mambo_wa_serikali_ya_nigeria_kuhusiana_na_hali_ya_sheikh_zakzaky
Familia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikificha na kukataa kutoa taarifa kuhusiana na hali ya kiafya ya kiongozi huyo pamoja na mkewe.
(last modified 2026-01-14T08:12:18+00:00 )
Oct 27, 2019 23:08 UTC
  • Ufichaji mambo wa serikali ya Nigeria kuhusiana na hali ya Sheikh Zakzaky

Familia ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imetangaza kuwa, serikali ya nchi hiyo imekuwa ikificha na kukataa kutoa taarifa kuhusiana na hali ya kiafya ya kiongozi huyo pamoja na mkewe.

Ofisi ya Sheikh Zakzaky imeinukuu familia ya kiongozi huyo na kuandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Twitter kwamba: Idara ya huduma za Serikali imekuwa ikificha mambo kuhusiana na hali ya kiafya ya Sheikh Ibrahim Zakzaky.

Ripoti zaidi zinasema kuwa, tangu Sheikh Zakzaky na mkewe wakatishe matibabu nchini India kutokana na mashinikizo na ukwamishaji mambo wa serikali ya Rais Muhammad Buhari na kulazimika kurejea Nigeria wamekuwa wakishikiliwa kinyume cha sheria mahala pasipojulikana.

Maandamano ya kushinikiza kuachiliwa huru Sheikkh Ibrahim Zakzaky

Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe walitiwa nguvuni tarehe 13 Desemba 2015 wakati askari wa jeshi la Nigeria walipovamia na kushambulia Hussainiyah iliyoko katika mji wa Zaria. Katika shambulio hilo, mamia ya Waislamu wa madhehebu ya Shia nchini Nigeria, wakiwemo watoto watatu wa kiume wa Sheikh Zakzaky, waliuawa shahidi.

Baada ya jitihada kubwa, maandamano ya kila pembe na mashinikizo mengi ya ndani na kimataifa, mnamo mwezi Agosti mwakka huu, mahakama ya Nigeria iliruhusu Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe wapelekwe India kutibiwa, lakini kutokana na matatizo na vizuizi vilivyowekwa na maafisa wa usalama walioandamana naye, kiongozi huyo wa kidini pamoja na mkewe waliamua kurudi Nigeria baada ya kukaa India kwa muda wa siku mbili tu pasi na kupatiwa matibabu.