Umoja wa Mataifa walaani jinai na ukatili wa magaidi nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i58100-umoja_wa_mataifa_walaani_jinai_na_ukatili_wa_magaidi_nchini_nigeria
Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kulaani vitendo vya ukatili na jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Nigeria iliyoko magharibi mwa Afrika.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Dec 25, 2019 09:11 UTC
  • Umoja wa Mataifa walaani jinai na ukatili wa magaidi nchini Nigeria

Umoja wa Mataifa umetoa taarifa na kulaani vitendo vya ukatili na jinai zinazofanywa na makundi ya kigaidi katika maeneo mbalimbali ya nchi ya Nigeria iliyoko magharibi mwa Afrika.

Taarifa ya Umoja wa Mataifa imeeleza kwamba, makundi ya kigaidii yamefanya ukatili mkubwa wa kuwanyonga raia wengi na kuwateka wengine katika moja ya miji ya kaskkazibni mwa nchi hiyo ambayo ni ngome za kundi la kigaidi la Boko Haram.

Stephane Dujarric, msemaji wa Antonio Guterres, Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema kuwa, matukio ya kunyongwa na kutekwa raia yamefanyika katika jimbo la Borno.

Umoja wa Mataifa umesisitiza kuwa, unalaani matukio hayo yaliyo dhidi ya ubinadamu na unataka kuchukuliwa hatua za kukabiliana na vitendo kama hivyo.

Wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram 

Kundi la kigaidi la Boko Haram lilianzisha shughuli zake za kigaidi mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria ambapo sasa limepanua wigo harakati zake hadi katika nchi za Niger, Chad na kaskazini mwa Chad.

Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, katika muongo mmoja wa harakati za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na wengine wanaokaribia milioni tatu wamekuwa wakimbizi.

Boko Haram ni kundi la kitakfiri lenye misimamo ya kufurutu mipaka nchini Nigeria ambalo kutokana na kuwa na ufahamu mbaya na potofu kuhusiana na Uislamu, limeitumbukiza nchi hiyo katika dimbwi la machafuko na mauaji pamoja na kuzusha hitilafu za kidini na kikabila nchini humo.

Serikali ya Nigeria inayoongoawa na Rais Muhamaduu Buhari inalaumiwa kwa kuzembea katika kukakabiliana na kundi hilo la kigaidi ambalo limesababisha maafa makubwa.