Jan 29, 2020 08:13 UTC
  • Watu 39 wauawa katika shambulio la kigaidi kaskazini mwa Burkina Faso

Watu 39 wameuawa katika shambulio la kigaidi lililofanywa kaskazini mwa Burkina Faso.

Serikali ya Burkina Faso imetangaza kuwa, shambulio hilo la kigaidi limefanywa katika kijiji kimoja kilichoko katika mkoa wa Soum kaskazini mwa nchi hiyo.

Wiki iliyopita pia watu 36 waliuawa na wengine watatu walijeruhiwa katika shambulio la kigaidi lililolenga soko la kijiji cha Alamo mkoani Sanmatenga kaskazini mwa nchi hiyo. Baada ya kufanya hujuma hiyo, washambuliaji waliliteketeza kwa moto pia soko hilo.

Burkina Faso, kama zilivyo nchi jirani za Mali na Niger imekuwa ikiandamwa na mashambulio ya kigaidi ya mara kwa mara, ambapo tangu mwaka 2015 hadi sasa watu 750 wameshauawa na wengine zaidi ya 560,000 wamelazimika kuyahama makazi yao kutokana na mashambulio hayo.

Umoja wa Mataifa umetangaza kuwa, mashambulio ya kigaidi yaliyofanywa katika eneo la magharibi mwa Afrika katika mwaka uliomalizika wa 2019 yameua raia elfu nne wa nchi za eneo hilo.../

Tags