Nigeria: Watu 47 wauawa na 'majambazi' katika jimbo la Katsina
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60490-nigeria_watu_47_wauawa_na_'majambazi'_katika_jimbo_la_katsina
Vyombo vya usalama nchini Nigeria vimetangaza kuwa, kwa akali watu 47 wameuawa katika shambulio la majambazi wenye silaha dhidi ya vijiji kadhaa katika jimbo la Katsina, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 20, 2020 07:19 UTC
  • Nigeria: Watu 47 wauawa na 'majambazi'  katika jimbo la Katsina

Vyombo vya usalama nchini Nigeria vimetangaza kuwa, kwa akali watu 47 wameuawa katika shambulio la majambazi wenye silaha dhidi ya vijiji kadhaa katika jimbo la Katsina, kaskazini mashariki mwa nchi hiyo.

Taarifa ya polisi ya Nigeria inaeleza kuwa, mashambulizi hayo yalitokea katika wilaya za Dutsenma, Danmusa na Safana kulingana na mkuu wa polisi wa eneo hilo.

Msemaji wa polisi wa serikali ya Jimbo la Katsina, Gambo Isah amesema kuwa, watu walio kuwa kwenye pikipiki walifanya "mashambulizi ya wakati mmoja" dhidi ya jamii tatu huko Katsina, na kuwa wakaazi 47.

Mauaji hayo yanaripotiwa huku Nigeria ikiendelea kusumbuliwa na ukosefu wa usalama na amani hasa katika maeneo ya kaskazini mashariki mwa nchi hiyo kufuatia harakati za wanamgambo wa kundi la kigaidi la Boko Haram.

Kwa mujibu wa ripoti za Umoja wa Mataifa, katika muongo mmoja wa shughuli za kundi la Boko Haram nchini Nigeria, zaidi ya watu elfu 30 wameuawa na wengine wanaokaribia milioni tatu wamekuwa wakimbizi.

Wanachama wa kundi la kigaidi la Boko Haram

Kundi la kigaidi na ukufurishaji la Boko Haram lilianzisha shughuli zake za kigaidi mwaka 2009 kaskazini mwa Nigeria ambapo hadi sasa limepanua wigo wake hadi katika nchi za Niger, Chad na kaskazini mwa Chad.

Serikali ya Nigeria inayoongozwa na Rais Muhamadu Buhari imeendelea kulaumiwa na kukosolewa kutokana na kuzembea katika kukakabiliana na kundi hilo la kigaidi ambalo limevuruga usalama wa nchi hiyo na nchi za jirani.