Wauguzi wagoma Malawi wakati wa janga la corona
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i60530-wauguzi_wagoma_malawi_wakati_wa_janga_la_corona
Mgomo wa kitaifa wa wauguzi nchini Malawi umekwamisha shughuli katika hospitali za umma wakati huu ambapo nchi hiyo inapambana na ugonjwa wa corona au Covid-19.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Apr 22, 2020 03:32 UTC
  • Wauguzi wagoma Malawi wakati wa janga la corona

Mgomo wa kitaifa wa wauguzi nchini Malawi umekwamisha shughuli katika hospitali za umma wakati huu ambapo nchi hiyo inapambana na ugonjwa wa corona au Covid-19.

Wauguzi hao wanalalamikia mazingira magumu ya kufanyia kazi na kukosa vifaa vya kujilinda. Baadhi ya madaktari pia wanaripotiwa kugoma.

Wauguzi nchini Malawi wamegoma kulalamikia hatua ya serikali kushindwa kuwaajiri wauguzi zaidi na kuwapa vifaa vya kujilinda wakati huu wa janga la Corona.

Serikali ilikuwa imeahidi kuwaajiri maafisa 2000 wa afya ili kudhibiti maambukizi ya ugonjwa wa Corona.

Lango la Hospitali Kuu ya Kamuzu nchini Malawi

Hadi sasa watu 18 vimethibitishwa kuambukizwa corona nchini Malawi ambapo watu wawili wamefariki na wengine watatu wamepata afueni. Watu wa Malawi sasa wanahofu kuwa huenda idadi ya visa vya maambukizi ya virusi vya Corona ikaongezeka kutokana na hali ngumu inayowakabili wananchi wa taifa hilo.

Katika Hospitali ya Kamuzu Central iliyo katika mji mkuu Lilongwe, wagonjwa wamelazimika kurudi nyumbani baada ya kukosa huduma