Misri na Ethiopia zaafikiana juu ya maji ya bwana la al Nahdha
Misri na Ethiopia zimeafikiana juu ya jinsi ya kujaza maji katika bwana lililozusha mgogoro mkubwa baina ya pande hizo mbili la al Nahdha.
Duru za kuaminika za Sudan zimeripoti kuwa, maafisa wa Misri na Ethiopia wamekubaliana na pendekezo lililotolewa na Sudan kuhusiana na masuala ya kiufundi ya kujaza maji katika bwawa la al Nahdha baada ya hitilafu kubwa zilizosababisha mgogoro na malumbano baina ya Cairo na Addis Ababa.
Nchi mbili za Misri na Sudan zinapinga mradi wa ujenzi wa bwawa la al Nahdha juu ya maji ya Mto Nile zikisema kuwa, ujenzi huo unapunguza mgao wa maji wa nchi hizo. Mgogoro huo umepamba moto kiasi cha Misri kutishia kutumia nguvu za kijeshi kwa ajili ya kuzuia ujenzi huo.
Bwawa la al Nahdha linajengwa katika Mto Nile nchini Ethiopia na katika umbali wa kilomita 40 kutoka mpaka wa Sudan. Ethiopia ilianza kujenga bwawa hilo mwezi Apili mwaka 2011, hata hivyo hitilafu kali kati yake na Misri na Sudan zimechelewesha ujenzi wake.