Ouattara ateuliwa na chama chake kuwani tena urais Ivory Coast
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i62512-ouattara_ateuliwa_na_chama_chake_kuwani_tena_urais_ivory_coast
Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast ameteuliwa tena na chama chake kuwania urais kwa muhula wa tatu ingawa binafsi hajachukua uamuzi kuhusu jambo hilo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jul 30, 2020 10:49 UTC
  • Ouattara ateuliwa na chama chake kuwani tena urais Ivory Coast

Rais Alassane Ouattara wa Ivory Coast ameteuliwa tena na chama chake kuwania urais kwa muhula wa tatu ingawa binafsi hajachukua uamuzi kuhusu jambo hilo.

Akizungumza mbele ya maafisa wa ngazi za juu wa chama tawala cha RHDP  waliokutana mjini Abidjan Jumatano, Ouattara amesema atazingatia maamuzi ya chama chake kabla ya kutangaza msimamo wake. Aidha amesema atalihutubia taifa hivi karibuni huku akisisitiza kuwa anataka kuona chama cha RHDP kinashinda uchaguzi.

Aidha amewataka wanachama wa RHDP waendelee kumuenzi Amadou Gon Coulibaly na wampe muda wa kupumzika na kutafakari.

Tangu kifo cha Waziri Mkuu Amadou Gon Coulibaly mapema mwezi Julai, wajumbe mbalimbali kutoka chama cha RHDP wamekuwa wakimshinikiza rais Ouattara kuwania uchaguzi wa urais wa mwezi Oktoba.

Uchaguzi huo wa Oktoba unatarajiwa kuwa na ushindani mkali tangu mwaka 2010 baada ya ushindi wa Ouattara dhidi ya Laurent Gbagbo, ushindi uliochochea vita vilivyosababisha vifo vya watu 3,000.

Laurent Gbagbo

Ouattara mwenye umri wa miaka 77 amewahi kunukuliwa akisema, anakusudia kukabidhi madaraka kwa kizazi cha vijana, lakini pia anasisitiza kwamba, mabadiliko ya katiba ya mwaka 2016 yaliondoa kikomo cha muhula wa urais yanampa fursa ya kuwania tena kwa mara ya tatu. Wapinzani Ivory Coast wanasisitiza kuwa Ouattara hapaswi kugombea tena urais.