Askari usalama washambulia waombolezaji katika kumbukumbu ya Ashura nchini Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63127-askari_usalama_washambulia_waombolezaji_katika_kumbukumbu_ya_ashura_nchini_nigeria
Askari usalama nchini Nigeria jana viliwashambulia waombolezaji katika kumbukumbu ya Ashura na kuwajeruhi kadhaa miongoni mwao.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Aug 30, 2020 22:05 UTC
  • Askari usalama washambulia waombolezaji katika kumbukumbu ya Ashura nchini Nigeria

Askari usalama nchini Nigeria jana viliwashambulia waombolezaji katika kumbukumbu ya Ashura na kuwajeruhi kadhaa miongoni mwao.

Waislamu wa Kishia nchini Nigeria jana waliungana na mamilioni ya wafuasi wengine wa Ahlul-Baiti (as) duniani kote katika kumbukumbu ya mauaji ya mjukuu wa Mtume SAW, Imam Hussein AS ambapo maeneo zaidi ya 300 nchini humo yalihuisha kumbukumbu hiyo.

Hata hivyo kama kawaida, askari usalama nchini Nigeria ambao wamekuwa wakiwakandamiza Waislamu wa Kishia nchini humo waliwashambulia waombolezaji hao wa Ashura na kuwajeruhi kadhaa miongoni mwao.

Shambulio la jana limefuatia lile la juzi katika siku ya kumbukumbu ya Tasua ambapo polisi ya jimbo la Kaduna iliwashambulia Waislamu waliokuwa katika maombolezo ya Imam Hussein na kuwaua shahidi watatu kati yao.

Mauaji dhidi ya Waislamu yaliyofanywa na vikosi vya usalama vya Nigeria katika mji wa Zaria mwaka 2015

Taarifa zaidi zinasema kuwa, licha ya vizuizi kadhaa vilivyowekwa na serikali ya Nigeria, hafla za maombolezo mwaka huu pia zimefanyika katika barabara za miji ya Kaduna, Sokoto na Zaria. 

Washiriki wa maombolezo ya Imam Hussein AS wametangaza upinzani wao pia dhidi ya hatua ya kufanya mapatano na utawala haramu wa Israel.

Kadhalika waombolezaji hao wa Imam Hussein AS wameshiriki kwenye kampeni ya uchangiaji damu na wakaitaka serikali ya Nigeria inayoongozwa na Rais Muhamadu Buhari imwachie huru Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya nchi hiyo Sheikh Ibrahim Zakzaky ambaye anashikiliwa kizuizini tangu mwaka 2015.