Maelfu ya Wamisri wakamatwa katika maandamano dhidi ya utawala wa Sisi
(last modified Sun, 11 Oct 2020 12:02:49 GMT )
Oct 11, 2020 12:02 UTC
  • Maelfu ya Wamisri wakamatwa katika maandamano dhidi ya utawala wa Sisi

Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limesema kwa uchache watu elfu mbili wametiwa mbaroni katika maandamano ya kupinga utawala wa Rais Abdel Fattah al-Sisi wa Misri ndani ya siku 20 zilizopita.

Shirika hilo limeitaka serikali ya al-Sisi iwaachie huru wanachi hao waliokamatwa wakishiriki maandamano likisisitiza kuwa, mkusanyiko na maandamano ya amani ni haki ya msingi katika nchi yoyoye ile inayodai kuwa ina demokrasia.

Kwa wiki kadhaa sasa, waandamanaji hao wamekuwa wakijitokeza mitaani na kulalamikia matatizo yao ya kiuchumi na kijamii licha ya kutambua hatari kubwa ya kupoteza maisha au usalama wao. 

Maafisa usalama wanaokandamiza maandamano ya amani ya wananchi wa Misri

Makundi ya kutetea haki za binadamu yanasema kuwa, mbali na kutiwa mbaroni, Wamisri kadhaa pia wameuawa tangu walipoanza maandamano hayo ya kupinga utawala wa rais wa nchi hiyo tarehe 20 mwezi uliopita wa Septemba. 

Tangu aliposhika madaraka ya nchi kupitia mapinduzi ya kijeshi hapo mwaka 2013, Abdel Fattah al-Sisi amekuwa akikandamiza harakati zote za wapinzani wa serikali akiungwa mkono au kunyamaziwa kimya na nchi za Magharibi hususan Marekani. 

Tags