Sudan yaikosoa Marekani kwa kukwamishwa kufikiwa demokrasia huko Khartoum
(last modified Mon, 12 Oct 2020 07:35:17 GMT )
Oct 12, 2020 07:35 UTC
  • Sudan yaikosoa Marekani kwa kukwamishwa kufikiwa demokrasia huko Khartoum

Waziri Mkuu wa Sudan ameituhumu Marekani kuwa inaikwamisha Sudan kufikia demokrasia.

Abdallah Hamdok amesema kuwa vikwazo vya Marekani dhidi ya Sudan vilivyoanza tangu jina la Sudan lilipowekwa katika orodha ya ugaidi mwaka 1993 vimelemaza uchumi wa nchi hiyo. Amesema hakuna dhamama yoyote ya kuendelezwa demokrasia hadi kufanyika uchaguzi mwaka 2022. 

Marekani iliiwekea vikwazo Sudan kwa kisingizio kwamba nchi hiyo ilimpatia hifadhi Usama bin Laden kiongozi wa mtandao wa al Qaida kuanzia mwaka 1993 hadi 1996. Waziri Mkuu wa Sudan ameongeza kuwa bin Laden alifukuzwa nchini humo zaidi ya miaka 20 iliyopita; na Wasudani mwezi Aprili mwaka jana waliuondoa madarakani utawala wa Omar al Bashir ambao ulimuhifadhi Bin Laden. Amesema wananchi wa Sudan hawajawahi kuwa magaidi. 

Usama bin Laden, aliyekuwa kiongozi wa mtandao wa kigaidi wa al Qaida 

Abdallah Hamdok aidha amekadhibisha baadhi ya tetesi kwamba itaitambua rasmi Israel iwapo Sudan itaondolewa kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono ugaidi. Mwaka 1997 Marekani iliiweka Sudan kwenye orodha ya nchi zinazounga mkono makundi ya kigaidi na kisha kuiwekea vikwazo vya kiuchumi na kijeshi. Tarehe 6 Oktoba mwaka 2017 Washington na serikali ya Khartoum zilifikia mapatano ya kuiondolea Sudan vikwazo hivyo vya kiuchumi. Hata hivyo, kivitendo hadi sasa vikwazo hivyo havijaondolewa. 

Tags