Watu wenye silaha wameua watu wasiopungua 12 kaskazini mwa Nigeria
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i63971-watu_wenye_silaha_wameua_watu_wasiopungua_12_kaskazini_mwa_nigeria
Watu kadhaa waliokuwa na silaha wamevamia vijiji viwili kaskazini mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua 12 na kujeruhi wengine 8.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 12, 2020 04:13 UTC
  • Watu wenye silaha wameua watu wasiopungua 12 kaskazini mwa Nigeria

Watu kadhaa waliokuwa na silaha wamevamia vijiji viwili kaskazini mwa Nigeria na kuua watu wasiopungua 12 na kujeruhi wengine 8.

Uvamizi huo ulijiri Ijumaa na Jumamosi iliyopita katika vijiji viwili vya Kidandan na Kadai katika jimbo la Kaduna kaskazini mwa Nigeria. Duru za ndani zimeripoti kuwa, idadi kubwa ya watu waliokuwa na silaha walishuhudiwa katika uvamizi huo. Ali Naduma Seneta wa bunge la Nigeria aliwahi kuashiria kwamba mamluki wa kundi la kigaidi la Boko Haram wamewaua watu 75 katika eneo la Gwoza katika jimbo la Borno; na kutahadharisha juu ya hali hatari ya eneo hilo.  

Seneta huyo wa Nigeria alieleza kuwa, mbali na mashambulizi ya Boko Haram wakazi wa eneo hilo wanakabiliwa na njaa na kusema hali ya raia hao itakuwa mbaya sana iwapo wanaharakati na taasisi za kiraia hazitachukua hatua katika uwanja huo. 

Magaidi wa Boko Haram  

Kwa muda sasa Nigeria inakabiliana na mashambulizi ya kigaidi ya kundi la Boko Haram; na ingali inasumbuliwa na hujuma na mashambulizi ya mara kwa mara ya kundi hilo licha ya serikali kufanya juhudi za kukabiliana na kundi hilo.