Makumi wauawa Somalia katika mapigano ya wanajeshi na magaidi wa al Shabab
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64055-makumi_wauawa_somalia_katika_mapigano_ya_wanajeshi_na_magaidi_wa_al_shabab
Makumi ya wanajeshi na magaidi wameuawa katika mapigano ya siku mbili baina ya askari wa jeshi la serikali ya Somalia na magaidi wa kundi la al Shabab kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Mogadishu.
(last modified 2026-04-19T09:26:01+00:00 )
Oct 16, 2020 10:16 UTC
  • Makumi wauawa Somalia katika mapigano ya wanajeshi na magaidi wa al Shabab

Makumi ya wanajeshi na magaidi wameuawa katika mapigano ya siku mbili baina ya askari wa jeshi la serikali ya Somalia na magaidi wa kundi la al Shabab kaskazini magharibi mwa mji mkuu, Mogadishu.

Shirika ramsi la habari la Somalia, Sonna, limeripoti Ijumma kuwa wanajeshi wamefanikiwa kuwaua magaidi 50 wa kundi la al Shabab katika mapigano yaliyojiri eneo la Afgoye.. Walioshuhudia mapigano hayo wanasema makumi ya askari wa Somalia waliuawa kama ambavyo pia makumi ya magaidi wa al Shabab nao pia waliuawa. Shirika rasmi la habari la Somalia limesema miongoni mwa magaidi waliouawa alikuwemo Osman il Fidow ambaye alikuwa kamanda wa ngazi za juu wa al Shabab.

Tangu mwaka 2007, kundi la kigaidi la al-Shabaab lenye mfungamano na mtandao wa al Qaida limekuwa likifanya mashambulizi ndani ya Somalia kwa lengo la kuiangusha serikali kuu ya nchi hiyo inayoungwa mkono na Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.

Askari wa AMISOM 

 

Jeshi la Somalia kwa kusaidiwa na kikosi maalumu cha Umoja wa Afrika AMISOM lilifanikiwa kuwafurusha magaidi wa al Shabab katika mji mkuu Mogadishu, mwezi Agosti 2011.

Hata hivyo bado wanamgambo hao wanadhibiti maeneo ya vijijini ya kusini na katikati mwa Somalia na wanafanya mashambulizi ya mara kwa mara ya kuvizia katika mji mkuu Mogadishu na maeneo mengine.