Kubuniwa baraza jipya la mawaziri Somalia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i64131-kubuniwa_baraza_jipya_la_mawaziri_somalia
Waziri Mkuu wa Somalia ametangaza habari ya kubuniwa baraza jipya la mawaziri la nchi hiyo ambapo baadhi ya mawaziri wa zamani wamejumuishwa.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Oct 20, 2020 08:25 UTC
  • Kubuniwa baraza jipya la mawaziri Somalia

Waziri Mkuu wa Somalia ametangaza habari ya kubuniwa baraza jipya la mawaziri la nchi hiyo ambapo baadhi ya mawaziri wa zamani wamejumuishwa.

Mohamed Hussein Roble, Waziri Mkuu wa Somalia alitangaza habari hiyo hapo jana Jumatatu na kuongeza kuwa baraza hilo litakuwa na mawaziri 44.

Ofisi ya waziri mkuu huyo imetoa taarifa ikisema kuwa baraza hilo litakuwa na mawaziri 27, mawaziri washauri 17 na manaibu waziri 26.

Tarifa hiyo imesema kwamba mawaziri wa zamani ambao wataendelea kuhudumu katika nafasi zao katika baraza hilo jipya la mawaziri ni watatu ambao ni Ali Abdurahman Diali, Ahmed Isse Awad na Fauzia Abikar ambao watahudumu kwa utaratibu kama mawaziri wa fedha, mambo ya nje na afya.

Mohamed Hussein Roble, Waziri Mkuu wa Somalia

Rais Muhammaf Abdallah Farmaajo wa Somalia mwezi Julai uliopita alimteua Mohamed Hussein Roble kuwa waziri mkuu mpya wa nchi hiyo na kumpa jukumu la kubuni baraza la mawaziri.

Bunge la Somalia tarehe 25 mwezi huo huo lilipiga kura ya kutokuwa na imani na serikali ya Hassan Ali Khaire, hatua ambayo ilipitishwa na Rais Farmaajo.

Somalia inakabiliwa na tatizo kubwa la ukosefu wa amani na usalama kutokana na mashambulio ya mara kwa mara ya kundi la kigaidi la ash-Shabaab.