Wasudan waandamana kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanaharakati wa kisiasa
(last modified Wed, 30 Dec 2020 15:53:15 GMT )
Dec 30, 2020 15:53 UTC
  • Wasudan waandamana kufuatia kifo cha kutatanisha cha mwanaharakati wa kisiasa

Mamia ya wananchi wa Sudan wamefanya maandamano katika mji mkuu Khartoum na mji wa Omdourman kulalamikia kifo cha kutatanisha cha mwanaharakati mmoja wa kisiasa.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya al-Alam, maandamano hayo yamefanyika kufuatia kifo cha mwanaharakati mashuhuri wa nchi hiyo, anayefahamika  kama Bahaullah al-Nuri.

Bahaullah al-Nuri aliripotiwa kutekwa na askari wa kikosi cha dharuru ya haraka wiki mbili zilizopita. Waandamanaji hao wametoa mwito wa kulipizwa kisasi cha mauaji ya mwanaharakati huyo.

Maziko ya mwanaharakati huyo wa kisiasa wa Sudan yamegeuka na kuwa maandamano makubwa ya kulaani mauaji yake. Mwili wa mwendazake unaonesha kuwa aliteswa vibaya kabla ya kuuawa.

Al-Nuri alikuwa mwanachama wa Kamati ya Muqawama wakati wa maandamano yalimuondoa madarakani rais wa zamani wa nchi hiyo, Omar al-Bashir.

Maandamano yaliyomuondoa madarakani al-Bashir

Mpinzani huyo wa serikali nchini Sudan alitekwa nyara Disemba 16 kusini mwa Khartoum, na kisha mwili wake ukapatika siku tano baadaye katika Hospitali ya Omdourman.

Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Sudan imethubitisha katika ripoti yake ya uchunguzi kuwa mwanaharakati huyo wa kisiasa aliaga dunia kutokana na athari za kugongwa kichwani na kifaa butu.

Tags