Marufuku ya kupaa katika anga ya Qadarif nchini Sudan
(last modified Fri, 15 Jan 2021 07:05:48 GMT )
Jan 15, 2021 07:05 UTC
  • Marufuku ya kupaa katika anga ya Qadarif nchini Sudan

Maafisa wa Sudan wameanza kutekeleza sheria ya kuzuia ndege kupaa kwa masafa yaliyoainishwa katika anga ya mkoa wa Qadarif.

Kwa mujibu wa kanali ya televisheni ya Sky News ya Kiarabu, uamuzi uliochukuliwa unapiga marufuku ndege zote kuruka chini ya futi 29,000 katika anga ya Qadarif.

Uongozi wa ndege wa Sudan umetangaza kwamba uamuzi wa kutekeleza marufuku hiyo umefikiwa baada ya ndege za kivita za Ethiopia kukiuka anga ya Sudan.

Awali serikali ya Khartoum ilisema kuwa ndege za kijeshi za Ethiopia zilichukua hatua hatari ya kukiuka kwa makusudi anga ya Sudan na kutoa onyo kali dhidi ya kukaririwa kitendo hicho.

Mgogoro wa Sudan na Ethiopia

Nchi mbili hizo jirani zimekuwa na tofauti za mipaka za miaka mingi na hadi sasa hazihafanikiwa kuzitatua.

Ni wazi kuwa kuendelea tofauti hizo kunaweza kuhatarisha usalama wa eneo zima la Pembe ya Afrika na hasa ikitiliwa maanani kwamba Ethiopia inakabiliwa na mgogoro mwingine wa ndani katika eneo la Tigray na wakati huo huo kuzozana na majirani zake kuhusiana na ujenzi wa Bwawa la an-Nahdha, ambapo Sudan na Misri zinagombana na serikali ya Addis Ababa kwa kuhofia kupungukiwa na maji ya Mto Nile.

Tags