Mke wa Sheikh Zakzaky aambukizwa corona akiwa kifungoni
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i65996-mke_wa_sheikh_zakzaky_aambukizwa_corona_akiwa_kifungoni
Mtoto wa Sheikh Ibrahim Zakzaky Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa mama yake amepatwa na maambukizi ya corona wakati ambapo yupo jela.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Jan 23, 2021 04:59 UTC
  • Mke wa Sheikh Zakzaky aambukizwa corona akiwa kifungoni

Mtoto wa Sheikh Ibrahim Zakzaky Katibu Mkuu wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria amesema kuwa mama yake amepatwa na maambukizi ya corona wakati ambapo yupo jela.

Muhammad Ibrahim Zakzaky ameeleza kuwa, mama yake yupo jela na ameambukizwa corona huku  hali yake ikiwa mbaya. Muhammad Zakzaky ameongeza kuwa, mama yake angali anashikiliwa katika jela kuu iliyopo katika mji wa Kaduna nchini Nigeria; na hadi sasa bado hajafikishwa hospitalini kwa ajili ya matibabu. Sheikh Ibrahim Zakzaky na mkewe walitiwa mbaroni tarehe 13 Disemba mwaka 2015 katika shambulizi lililofanywa na wanajeshi wa Nigeria katika Husseiniya katika mji wa Zaria nchini humo. 

Sheikh Ibrahim Zakzaky 

Wakati wa kumtia mbaroni Sheikh Ibrahim Zakzaky jeshi la Nigeria liliwafyatulia risasi watu waliokuwa wamekusanyika kwenye Husseiniya hiyo na katika nyumba ya mwanazuoni huyo na kusababisha vifo vya mamia ya watu wakiwemo watoto watatu wa Sheikh Zakzaky.

Katika miezi ya karibuni wananchi wa Nigeria wamefanya maandamano mara kadhaa katika miji mbalimbali ya nchi hiyo wakitaka kuachiwa huru Sheikh Zakzaky hata hivyo askari usalama wa nchi hiyo mara zote wamekuwa wakikabiliana vikali na maandamano hayo.