Sharti la Ethiopia kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Sudan
(last modified Fri, 29 Jan 2021 02:08:36 GMT )
Jan 29, 2021 02:08 UTC
  • Sharti la Ethiopia kwa ajili ya kufanya mazungumzo na Sudan

Ethiopia imetangaza kuwa Sudan inapasa kuondoa wanajeshi wake katika maeneo yenye hitilafu baina ya Addis Ababa na Khartoum ili kufanya mazungumzo nayo.

Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Ethiopia ametangaza kuwa, nchi hiyo inaheshimu kupatiwa ufumbuzi kwa njia ya amani hitilafu zilizoko kati ya nchi hiyo na Sudan; na kwamba haitafanya mazungumzo yoyote na Sudan kuhusu suala la mipaka kabla ya Sudan kuondoa wanajeshi wake katika maeneo hayo ya mpaka yanayozozaniwa. 

Hii ni katika hali ambayo, Abdulfattah al Burhan Mkuu wa Baraza la Uongozi la Sudan amesema kuwa wanajeshi wa nchi hiyo wamejipanga upya ndani ya mipaka ya Sudan. 

Abdulfattah al Burhan, Mkuuwa baraza la uongozi la Sudan  

Wanajeshi wa Sudan katika siku za karibuni wamepigana kwa mara kadhaa na wenzao wa Ethiopia; na pande mbili hizo kushambuliana kila upande. 

Hitilafu kati ya Sudan na Ethiopia kuhusu ardhi ya kilimo huko al Fashaga eneo linalopatikana katika mpaka wa kimataifa wa Sudan ni eneo linalotumiwa na wakulima wa Ethiopia aambao wameishi hapo kwa miaka kadhaa sasa. 

Wanamgambo wa Kiethiopia karibu miaka 26 iliyopita walivamia ardhi za wakulima wa Sudan katika eneo hilo la al Fashaga na kisha ikawatoa kwa nguvu katika mashamba yao kwa kutumia silaha na kuzidhibiti ardhi hizo.

Serikali ya Khartoum inalituhumu jeshi la Ethiopia kuwa linawaunga mkono wanamgambo hao. 

Tags