Kuongezeka ugaidi Nigeria; mamia ya wanafunzi watekwa nyara
(last modified Sun, 28 Feb 2021 08:52:52 GMT )
Feb 28, 2021 08:52 UTC
  • Kuongezeka ugaidi Nigeria; mamia ya wanafunzi watekwa nyara

Mashambulio ya kigaidi yangali yanaendelea katika nchi za magharibi mwa Afrika na hasa nchini Nigeria. Katika mashambulio ya karibuni kabisa, mamia ya wanafunzi wametekwa nyara nchini humo kufuatia shambulio lililofanywa na wabeba silaha katika shule moja katika jimbo la Zamfara, kaskazini mwagharibi mwa nchi hiyo.

Katika miezi kadhaa iliyopita, makundi hayo yameimarisha shughuli zao za kigaidi katika nchi za eneo la magharibi na Sahel barani Afrika. Kundi la Boko Haram ni moja ya makundi ya kigaidi ambayo yameimarisha harakati zao za kuteka nyara wanafunzi huko Nigeria. Mbali na kuua makumi ya raia wasio na hatia, kundi hilo limekuwa likiteka nyara wanafunzi wa shule wakiwemo wasichana na wavulana, kama tilivyoshuhudia katika miezi ya karibuni ambapo magaidi walishambulioa shule moja katika jimbo la Katsina, kaskazini mwa Nigeria na kuteka nyara wanafunzi 300. Hivi sasa kundi hilo limeteka nyara tena wavulana wengine 300.

Boko Haram inaharamisha masomo kwa wanafunzi, na hilo lilithibitishwa wazi na kiongozi wa kundi hilo aliyetoa ujumbe wa sauti akisema wazi kuwa lengo la kushamabuliwa shule moja ya bweni katika mkoa wa Katsina lilikuwa ni kupambana na masomo ya Kimagharibi. Hata kama serikali ya Abuja imekuwa ikifanya juhudi kubwa za kuachiliwa huru wanafunzi hao lakini hadi sasa haijafanikiwa katika hilo.

Baadhi ya wanafunzi wa kike waliotekwa nyara na Boko Haram

Kwa kuteka nyara wanafunzi, magaidi wa Boko Haram wanakusudia kuibua wahka na hofu miongoni mwa raia na wakati huo huo kuwatumia wanafunzi kama askari wao wa vita. Wengi wa wanafunzi waliotekwa nyara wamekuwa wakitumika katika shughuli za uagidi na kujilipua baada ya kupewa mafunzo maalumu ya kijeshi.

Makundi ya kigaidi yanaendesha shughuli zao za uagidi kwa madhara ya watu wa Nigeria katika hali ambayo Rais Muhammadu Buhari wa nchi hiyo katika kapmeni zake za uchaguzi aliahidi kuyatokomeza kabisa makundi hayo na kurejesha amani na usalama katika nchi hiyo. Licha ya kuwa amekuwa madarakani kwa muda mrefu sasa lakini hadi hajawasilisha mpango wowote wa muda mrefu wa kupambana na makundi hayo, bali ametosheka tu kwa kupiga nara zisizotekelezwa kivitendo.

Katika miaka ya karibuni serikali ya Nigeria imeimarisha uhusiano wake wa kisiasa na kiuchumi na nchi kama vile Saudia Atrabia na ili kunufaika na utajiri wa nchi hizo, imekuwa ikitekeleza siasa ambazo zinalinda maslahi ya nchi hizo bila kujali iwapo zinadhuru maslahi ya raia wa nchi hiyo au la.

Madawi bin Muhammad ar-Rasheed, mhadhiri katika Kituo cha Utafiti wa Masuala ya Kisiasa na Kicumi ya Mashariki ya Kati kilicho na makao yake mjini London Uingereza anasema: Kuongezeka haraka barani Afrika makundi ya kigaidi kama Boko Haram nchini Nigeria na nchi jirani, ni jambo ambalo limewezekana kupitia msaada wa kilojestiki, kifedha na kisilaha wa moja kwa moja kutoka serikali ya Saudia.

Rais Muhammadu Buhari

Kwa hakika serikali ya Nigeria imeazimia kutumia vibaya mapambano dhidi ya ugaidi kwa madhara ya Waislamu wa nchi hiyo, jambo ambalo linafuatiliwa kwa karibu na Saudi Arabia na washirika wake wa Magharibi.

Ofisi ya Sheikh Ibrahim Zakzaky, Kiongozi wa Harakati ya Kiislamu ya Nigeria imesema kuhusu suala hilo kwamba: Wanachama wa kundi la Boko Haram kamwe haliwakilishi Waislamu. Kundi hilo limeanzishwa na watu ambao wameazimia kuharibu sura ya amani ya Uislamu.

Magaidi barani Afrika wanatumika kama chombo cha nchi za Magharibi na washirika wao kwa ajili ya kupora utajiri wa Waafrika na kutumia vibaya nafasi za kijografia za nchi zao na hasa Nigeria. Kwa msingi huo si rahisi kwa serikali kama ya Nigeria na za nchi nyingine za Kiafrika kuchukua uamuzi madhubuti wa kupambana vilivyo na makundi ya kigaidi. Katika uwanja huo ni wanafunzi ndio wanaokuwa wahanga wakuu wa vitendo vya kigaidi vya makundi hayo.