Sudan yaituhumu Ethiopia kuwa inalipatia silaha kundi moja la waasi
Sudan imeituhumu serikali ya Ethiopia kuwa inalipatia silaha kundi moja la uasi ili kuudhibiti mji wa al Karmak huko kusini mashariki mwa Sudan.
Chombo kimoja cha kijeshi cha Sudan ambacho hakikutaka jina lake litajwe kimesema kuwa, serikali ya Ethiopia imemtumia kamanda Joseph Touka huku ikimtumia pia makombora ili kuukalia kwa mabavu mji wa al Karmak kwa lengo la kufelisha jitihada za jeshi la Sudan za kuipatia ufumbuzi mizozo ya maeneo ya mpakani.
Joseph Touka kamanda wa wanamgambo wa harakati ya al Shaabiyah chini ya uongozi wa Abdulaziz al Hilu amekuwa akipigana vita na serikali ya Sudan tangu mwaka 2011 katika majimbo mawili ya Kordofan ya kusini na Blue Nile huko kuksini mashariki mwa Sudan.
Ethiopia ambayo ina hitilafu nyingi na Sudan khususan kuhusu mzozo wa maeneo ya mpakani na bwawa la An Nahdhah bado haijatoa jibu lolote kuhusu tuhuma hizo dhidi yake.