Wasudan waandamana wakitaka haki kwa waliouawa mwaka 2019
(last modified Fri, 04 Jun 2021 02:46:03 GMT )
Jun 04, 2021 02:46 UTC
  • Wasudan waandamana wakitaka haki kwa waliouawa mwaka 2019

Wananchi wa Sudan jana Alkhamisi walimiminika mabarabarani katika mji mkuu, Khartoum na miji mingine ya nchi hiyo, kushiriki maandamano ya kutaka kutendewa haki wahanga wa ghasia za mwaka 2019.

Watu wasiopungua 128 waliuawa na maafisa usalama katika maandamano ya kulilazimisha Baraza la Kijeshi la Mpito likabidhi madaraka kwa raia mnamo Juni 3 mwaka 2019. 

Maandamano ya jana mbali na kutaka kuwajibishwa maafisa usalama waliotumia mkono wa chuma dhidi ya waandamanaji, lakini yamefanyika pia kwa mnsaba wa mwaka wa pili wa kumbukumbu ya mauji hayo.

Maandamano ya jana yaliitishwa na Chama cha Wataalamu cha Sudan na Kamati za Muqawama ambazo zilikuwa na mchango mkubwa katika maandamano dhidi ya utawala wa aliyekuwa rais wa nchi hiyo, Omar al-Bashir.

Maandamano ya Wasudan

Sudan ilikumbwa na maandamano makubwa ya wananchi tangu Disemba 2018 yaliyopelekea kuanguka utawala wa karibu miaka 30 wa al-Bashir.

Jeshi la Sudan lilifanya mapinduzi mwezi Aprili mwaka uliofuata 2019, yaliyomng'oa madarakani Jenerali Omar al-Bashir kutokana na maandamano hayo makubwa ya wananchi.

Tags