Waliokuwa njiani kwenda kujiunga na al-Shabaab wakamatwa na polisi ya Kenya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i7177-waliokuwa_njiani_kwenda_kujiunga_na_al_shabaab_wakamatwa_na_polisi_ya_kenya
Polisi katika mpaka wa Kenya na Somalia wanawazuilia watu watano akiwemo mwanafunzi wa chuo cha walimu, kwa tuhuma za kwenda kujiunga na kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
May 16, 2016 03:49 UTC
  • Waliokuwa njiani kwenda kujiunga na al-Shabaab wakamatwa na polisi ya Kenya

Polisi katika mpaka wa Kenya na Somalia wanawazuilia watu watano akiwemo mwanafunzi wa chuo cha walimu, kwa tuhuma za kwenda kujiunga na kundi la kigaidi na kitakfiri la al-Shabaab.

Washukiwa hao wamekamatwa katika eneo la Wajir walipokuwa wanaelekea nchini Somalia. Kushikwa kwa watano hao kunafuatia kuimarishwa kwa operesheni za polisi dhidi ya kundi hilo, ambalo limekuwa likisajili wanachama wake wengi kutoka humu nchini. Al-Shabaab, hufanya usajili wake kupitia mitandao, kwa ushirikiano na mtandao wa kigaidi wa al-Qaeda na hivi karibuni baadhi ya wanachama wake wamedai kushirikiana na matakfiri wa Daesh ISIS.

“Kufuatia upenyo wa polisi katika mtandao wa usajili wa wanachama wa Al-Shabaab unaohusishwa na Bw Mohamed Mohamed Abdi na Nuseiba Mohamed Haji, polisi wameweza kuimraisha uchunguzi katika mitandao hiyo ambayo imekuwa chanzo kikuu cha kupotea kwa vijana wa humu nchini,” inasema ripoti ya serikali ambayo waandishi wa SwahiliHub waliiona.

Ripoti hiyo inaendelea kusema, “Ni kwa sababu ya juhudi tulizofanya, ambapo tumeweza kuwatia mbaroni vijana watano katika kaunti ya Wajir. Walipatikana wakiwa kwenye basi kuelekea Somalia kujiunga na kundi la kigaidi.”

Mamia ya vijana kutoka Kenya wamepotea katika siku za hivi karibuni, huku wengi wakishukiwa kujiunga na Al-Shaabab.