UN: Ukiukaji wa haki za binadamu unaendelea kufanyika nchini Burundi
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i74776-un_ukiukaji_wa_haki_za_binadamu_unaendelea_kufanyika_nchini_burundi
Kamisheni ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, hali ya haki za binadamu nchini Burundi bado ni ya maafa na mbaya sana licha ya Rais wa nchi hiyo kuahidi kuwa ataboresha hali hiyo.
(last modified 2026-02-21T22:51:18+00:00 )
Sep 17, 2021 22:01 UTC
  • UN: Ukiukaji wa haki za binadamu unaendelea kufanyika nchini Burundi

Kamisheni ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa imetangaza kuwa, hali ya haki za binadamu nchini Burundi bado ni ya maafa na mbaya sana licha ya Rais wa nchi hiyo kuahidi kuwa ataboresha hali hiyo.

Katika taarifa yake ya tano iliyotolewa siku ya Alkhamisi, Kamisheni ya Uchunguzi ya Umoja wa Mataifa Kuhusu Burundi imesema kuwa, hali jumla ya vyama vya siasa vya upinzani, waandishi habari na asasi zisizo za serikali zinazokandamizwa na vyombo vya dola imekuwa mbaya zaidi licha ya baadhi ya maboresho madogo.

Taarifa iliyotolewa na mkuu wa kamisheni hiyo ya Umoja wa Mataifa imesema, tangu Rais Évariste Ndayishimiye alipoapishwa kuwa kiongozi wa Burundi miezi 15 iliyopita, ukiukaji mkubwa wa haki za binadamu unaendelea kushuhudiwa nchini humo; na katika baadhi ya maeneo umekuwa mbaya zaidi. 

UN: Hali ya haki za binadamu ni mbaya sana nchini Burundi

Taarifa hiyo imesema kuwa, viongozi wa vyama vya upinzani wangali wanasumbuliwa na mbinyo, ukiukaji wa haki zao za binadamu, kupotezwa, kutiwa mbaroni na kuteswa. 

Burundi pia imeorodheshwa katika nafasi ya 147 kati ya nchi 180 katika ripoti ya Shirika la Maripota Wasio na Mpaka kuhusu uhuru wa waandishi habari.