Hali ya maafa yatangazwa Zimbabwe kufuatia ukame ulioikumba nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i763-hali_ya_maafa_yatangazwa_zimbabwe_kufuatia_ukame_ulioikumba_nchi_hiyo
Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametangaza hali ya maafa kufuatia ukame mkali ulioathiri maeneo mengi ya vijijini nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 07, 2016 04:17 UTC
  • Hali ya maafa yatangazwa Zimbabwe kufuatia ukame ulioikumba nchi hiyo

Rais Robert Mugabe wa Zimbabwe ametangaza hali ya maafa kufuatia ukame mkali ulioathiri maeneo mengi ya vijijini nchini humo.

Tangazo hilo linatazamiwa kukabiliwa na miitikio ya jamii ya kimataifa kwa ajili ya kutoa misaada ya chakula kwa Zimbabwe. Waziri wa Serikali za Mitaa na Ajira wa Zimbabwe amesema kuwa asilimia 26 ya jamii ya watu milioni 2.44 hivi sasa wanahitaji msaada wa chakula nchini humo kufuatia ukame mkali kuiathiri nchi hiyo. Vijiji vingi vya kusini mwa Zimbabwe vimepoteza mifugo ya ng'ombe na mazao kutokana na ukame mkubwa ulioikumba nchi hiyo.