Watatu wauawa katika hujuma ya anga Libya
Watu watatu wameuwawa katika hujuma ya ndege za kivita zisizojulikana nchini Libya.
Imearifiwa kuwa ndege hizo zisizojulikana leo zimedondosha mabomu katika mji wa bandarani wa Derna mashariki mwa Libya ambapo watu watatu akiwemo mama na matoto wake wamepoteza maisha. Ndege za kivita zisizojulikana kwa kawaida hulenga magaidi katika maeneo kadhaa ikiwa ni pamoja na Derna na mji wa Sirte ambao ni ngome ya magaidi wa ISIS.
Libya hivi sasa inakumbwa na mapingano baina ya serikali mbili zinazodai kuitawala nchi hiyo. Mirengo hiyo yote ina makundi ya wanamgambo. Umoja wa Mataifa unajaribu kupatanisha pande hizo ili zikubali serikali ya umoja wa kitaifa iliyopendekezwa hivi karibuni.
Libya imekuwa ikikumbwa na machafuko tokea dikteta wa zamani wa nchi hiyo Muammar Ghaddafi aangushwe madarakani miaka minne iliyopita.