Rais wa Algeria: Kuitetea Palestina ni kipaumbele cha serikali ya Algiers
-
Abdelmadjid Tebboune
Rais wa Algeria ametangaza kuwa nchi yake itaendelea kulitetea taifa la Palestina dhidi ya utawala ghasibu wa Israel.
Abdelmadjid Tebboune amesisitiza kuwa kuitetea Palestina ni katika vipaumbele vya serikali yake na kuongeza kuwa, hakuna upande wowote wa kigeni unaoweza kubadili msimamo huo wa Algeria.
Tebboune amesema, baadhi ya nchi zina woga kuhusu sera za kujitawala za Algeria na kuongeza kuwa, Waalgeria wataendeleza njia yao kwa irada na azma imara hadi nchi hiyo itakapofika kwenye nafasi yake halisi kikanda na kimataifa kwa msaada wa jeshi la kitaifa na wananchi wake.
Katika miezi ya hivi karibuni Algeria imekuwa mstari wa mbele kupinga sera na siasa za utawala ghasibu wa Israel na ukandaizaji wake dhidi ya wananchi wa Palestina.
Misimamo hiyo ya Algeria imeshuhudiwa zaidi baada ya jirani yake, Morocco, kutia saini makubaliano ya kuanzisha uhusiano wa kawaida na Israel na kutia saini hati ya kuanzisha ushirikiano wa kijeshi na utawala huo ghasibu.