Waliouawa katika hujuma pacha za mabomu Somalia wafika 48
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i81756-waliouawa_katika_hujuma_pacha_za_mabomu_somalia_wafika_48
Watu 48 wameuawa katika mashambulizi pacha ya mabomu katika mji wa Beledweyne katika eneo la Hiran, katikati ya Somalia. Watu wenine 108 wamejeruhiwa katika mahambulizi hayo pacha.
(last modified 2026-02-15T09:07:51+00:00 )
Mar 25, 2022 02:30 UTC
  • Waliouawa katika hujuma pacha za mabomu Somalia wafika 48

Watu 48 wameuawa katika mashambulizi pacha ya mabomu katika mji wa Beledweyne katika eneo la Hiran, katikati ya Somalia. Watu wenine 108 wamejeruhiwa katika mahambulizi hayo pacha.

Maafisa wa serikali ya Somalia walitangaza habari hiyo jana Alkhamisi na kuongeza kuwa, Mbunge mashuhuri Amina Mohammed Abdi na mbunge wa zamani wa nchi hiyo, Hassan Abdi ni miongoni mwa watu waliouawa katika hujuma hizo pacha zinazoaminika kuwa za kigaidi.

Vyombo vya habari vya Somalia vimeripoti kuwa, mtunga sheria huyo pamoja na walinzi wake kadhaa waliuawa nje ya makazi ya Rais wa eneo la HirShabelle Ali Gudlawe Hussein, katika kambi ya kijeshi ya Lama-Galay katika mripuko wa kwanza.

Habari zaidi zinasema kuwa, watu wengine zaidi ya 20 waliuawa katika shambulio la pili lililolenga gari la kijeshi lililokuwa limebeba majeruhi wa mripuko wa kwanza.

Shambulio la kigaidi nchini Somalia

Waziri Mkuu wa Somalia, Mohamed Hussein Roble amesema mashambulizi hayo pacha mjini Beledweyne, na shambulio jingie la juzi Jumatano katika Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Aden Adde katika mji mkuu wa Somalia, Mogadishu lililoua watu 6, yana mfungamano na yametekelezwa kwa mpangilio maalumu. Kiongozi wa mkoa wa Hirshabelle huko Somalia amesema kuwa wanamgambo wa al Shabaab wamedai kuwa wametekeleza mashambulio hayo ili kuwalenga wanasiasa kabla ya uchaguzi. 

 

the leader of Hirshabelle state said Thursday, with Al-Shabaab insurgents claiming they were targeting politicians ahead of elections.

Naye Rais wa zamani wa Somalia, Hassan Sheikh Mohamud amesema yumkini hujuma za Beledweyne hazijafanywa na magaidi na huenda lilikuwa shambulizi la kisiasa kwa kuwa ni msimu wa kampeni za kisiasa wakati huu; huku akitoa mwito kwa jamii ya kimataifa kusaidia katika uchunguzi wa mashambulizi hayo.