Marzouki alitaka jeshi la Tunisia kumuondoa madarakani rais wa nchi hiyo
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i82392-marzouki_alitaka_jeshi_la_tunisia_kumuondoa_madarakani_rais_wa_nchi_hiyo
Rais wa zamani wa Tunisia, Moncef Marzouki ametoa wito kwa jeshi na vikosi vya usalama vya nchi hiyo kuingilia kati na kumwondoa madarakani rais wa sasa, Kais Saied na kulikabidhi mamlaka bunge lililochaguliwa na wananchi hadi pale uchaguzi mpya uliohuru na wa haki utakapofanyika.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Apr 11, 2022 11:29 UTC
  • Moncef Marzouki
    Moncef Marzouki

Rais wa zamani wa Tunisia, Moncef Marzouki ametoa wito kwa jeshi na vikosi vya usalama vya nchi hiyo kuingilia kati na kumwondoa madarakani rais wa sasa, Kais Saied na kulikabidhi mamlaka bunge lililochaguliwa na wananchi hadi pale uchaguzi mpya uliohuru na wa haki utakapofanyika.

Al-Marzouki amesema kwamba Saied amepoteza uhalali na imani ya wananchi na kubainisha kuwa, vikosi vya usalama na jeshi vinafuatilia hali ya mambo nchini Tunisia.

Ameongeza kuwa: "Saied anaungwa mkono na Imarati na Saudi Arabia katika jitihada za kuangamiza mapinduzi ya wananchi yaliyotokea katika nchi kadhaa za Kiarabu." 

Rais huyo wa zamani wa Tunisia amelaani shambulio lililofanywa dhidi ya Sheikh Rached Ghannouchi, Spika wa Bunge lililovunjwa la Tunisia, akitangaza mshikamano wake kamili na wabunge walioswekwa jela na utawala wa Rais Kais Saied.

Moncef Marzouki

Amesisitiza kuwa, rais wa sasa wa Tunisia anachochea vurugu, kutoa tuhuma dhidi la kila mtu nayepinga utawala wake na watu wote waliopigana na dhulma na ukandamizaji na kuwaita wasaliti.”

Al-Marzouki amesisitiza kuwa, kwa hali ilivyo hivi sasa yumkini Tunisia ikatumbukia kwenye vita vya wenyewe kwa wenyewe. 

Mwishoni mwa mwezi uliyopita, Rais wa Tunisia alitangaza kuvunja Bunge muda mfupi baada ya chombo hicho kupitisha sheria ya kufuta hatua za dharura zilizotangazwa na kiongozi huyo Julai 25 mwaka jana.

Wakati huo, Rais huyo wa Tunisia alichukua uamuzi wa ghafla na wa kushangaza wa kusitisha shughuli za Bunge na kuwafuta kazi Spika na Waziri Mkuu wa nchi hiyo, na kisha akatwaa udhibiti wa masuala yote ya utendaji nchini humo.