Misri kutumia JCPOA kuishinikiza Israel ijiunge na NPT
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i883-misri_kutumia_jcpoa_kuishinikiza_israel_ijiunge_na_npt
Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 maarufu kama JCPOA yanatoa fursa ya kipekee kwa serikali ya Cairo kuushinikiza utawala haramu wa Israel kujiunga na mkataba wa NPT unaozuia utengenezaji, usambazaji na utumiaji wa silaha za atomiki.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Feb 09, 2016 04:12 UTC
  • Misri kutumia JCPOA kuishinikiza Israel ijiunge na NPT

Waziri wa Mambo ya Nje wa Misri amesema makubaliano ya nyuklia yaliyofikiwa kati ya Iran na kundi la 5+1 maarufu kama JCPOA yanatoa fursa ya kipekee kwa serikali ya Cairo kuushinikiza utawala haramu wa Israel kujiunga na mkataba wa NPT unaozuia utengenezaji, usambazaji na utumiaji wa silaha za atomiki.

Sameh Shoukry ameliambia jarida mashuhuri la Wall-street Journal la nchini Marekani kwamba, Misri inaunga mkono makubaliano ya nyuklia na kusisitiza kwamba makubaliano hayo ndiyo njia pekee ya kuhakikisha uthabiti na amani katika eneo la Mashariki ya Kati na duniani kwa ujumla. Hata hivyo amesema utulivu huo na amani havitapatikana madhali Israel inaendelea kumiliki mamia ya silaha hatari za nyuklia.

Itakumbukwa kuwa, mwaka uliopita Misri ilikuwa imependekeza kufanyika mkutano wa kimataifa wa kujadili makubaliano ya NPT lakini serikali ya Marekani ikapinga kufanyika kongamano hilo. Inaaminika kuwa utawala ghasibu wa Israel ndio ulioishinikiza Washington kuzuia kufanyika mkutano huo.

Takwimu zisizo rasmi zinaonyesha kuwa Israel ina zaidi ya vichwa 200 vya silaha za nyuklia kwenye hifadhi yake.