Kais Saied aahidi kufanyia marekebisho sheria ya uchaguzi Tunisia
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i89060-kais_saied_aahidi_kufanyia_marekebisho_sheria_ya_uchaguzi_tunisia
Baada ya patashika na mijadala mingi hatimaye Rais wa Jamhuri ya Tunisia, Kais Saied ametangaza kwamba atafanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo.
(last modified 2023-11-27T12:14:11+00:00 )
Oct 09, 2022 02:57 UTC
  • Kais Saied aahidi kufanyia marekebisho sheria ya uchaguzi Tunisia

Baada ya patashika na mijadala mingi hatimaye Rais wa Jamhuri ya Tunisia, Kais Saied ametangaza kwamba atafanya marekebisho ya sheria ya uchaguzi ya nchi hiyo.

Uamuzi huo umechukuliwa miezi miwili tu kabla ya uchaguzi wa Bunge uliopangwa kufanyika mwezi Disemba mwaka huu. 

Mwezi Septemba mwaka huu kiongozi huyo wa Tunisia alitangaza sheria mpya ya uchaguzi ambayo imepingwa vikali na kambi ya upinzani. 

Chini ya sheria hiyo mpya, wapigakura watachagua wagombea binafsi katika uchaguzi wa Disemba 17 badala ya kuchagua orodha ya chama kimoja - mabadiliko ambayo yatadhoofisha ushawishi wa vyama.

Harakati ya Ennahda imeionya kuhusu hatari ya harakati ya Rais Saied ya kurekebisha sheria ya ya uchaguzi.

Ennahda imeongeza kuwa: Watunisia wanapaswa kuunganisha pamoja juhudi zao za kukabiliana na mapinduzi na kuzidisha maandamano ya amani dhidi ya serikali.

Julai 25, 2021 pia Rais wa Jamhuri ya Tunisia, katika miezi ya hivi karibuni, Rais wa Jamhuri ya Tunisia, Kais Saied, amechukua hatua ambazo zimechochea hasira za vyama vingi na raia wa nchi hiyo. Kuvunjwa kwa bunge na kufutwa kinga ya wawakilishi, kuvunjwa kwa Baraza Kuu la Mahakama la Tunisia na pia pendekezo la kuandikwa katiba mpya ya Tunisia ni miongoni mwa hatua hizo zilizotajwa na wapinzani kuwa ni mapinduzi dhidi ya kkati ya nchi, huku wanasheria wakisisitiza kuwa, ni jitihada za Kais Saied za kuhodhi madaraka ya nchi.