Tahadhari kuhusu kuongezeka magaidi wa Daesh Libya
https://parstoday.ir/sw/news/africa-i94-tahadhari_kuhusu_kuongezeka_magaidi_wa_daesh_libya
Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametahadharisha kuhusu kushamiri uwepo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini humo.
(last modified 2023-11-27T08:44:11+00:00 )
Jan 27, 2016 23:43 UTC
  • Tahadhari kuhusu kuongezeka magaidi wa Daesh Libya

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya ametahadharisha kuhusu kushamiri uwepo wa kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini humo.

Martin Kobler, ametahadharisha kuwa mchakato wa kisaisa wa bunge la Libya umechukua muda mrefu sana na kwamba mazingira yaliyojitokeza yanaandaa uwanja wa kupanuka harakati za kundi la kigaidi na kitakfiri la Daesh nchini humo.

Mjumbe Maalumu wa Umoja wa Mataifa katika masuala ya Libya amesema mbele ya waandishi wa habari huko Tunis, mji mkuu wa Tunisia kwamba katika hali ambayo wanasiasa wanafanya majadiliano na mashauriano, watu wenye misimamo ya kufurutu ada wao hupanua harakati na hujuma zao. Martin Kobler ameongeza kwa kuzingatia jambo hilo, bunge la nchi hiyo ambalo limeidhinishwa na jamii ya kimataifa limepinga moja ya vipengee vya makubaliano ya amani. Kwa mujibu wa kipengee hicho, kamanda mwenye nguvu wa jeshi la Libya atauzuliwa katika wadhifa wake.