-
Katibu Mkuu wa UN aahidi Afrika kuwa na mwakilishi wa kudumu kwenye Baraza la Usalama
Feb 16, 2025 10:43Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema sio sawa kwa bara la Afrika kutokuwa na kiti cha mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, na ameahidi kufanya kazi na Umoja wa Afrika na nchi wanachama ili kuhakikisha kuwa nchi za Afrika zinapata mwakilishi wa kudumu katika Baraza la Usalama.
-
Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini: Tunapinga kufurushwa Wapalestina, hatutasalimu amri mbele ya vitisho vya Trump
Feb 16, 2025 10:42Waziri wa Mambo ya Nje wa Afrika Kusini, Ronald Lamola, amesema kuwa nchi za bara hilo zina msimamo mmoja juu ya haja ya kusuluhisha mgogoro wa Ukanda wa Gaza ndani ya suluhisho la mataifa mawili, akisisitiza kwamba Pretoria haitarudi nyuma kuhusiana na msimamo wake katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki.
-
Mkuu wa jeshi la Uganda atishia kuushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo
Feb 16, 2025 05:44Jenerali Muhoozi Kainerugaba Mkuu wa jeshi la Uganda jana aliandika katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa X kuwa nchi hiyo itaushambulia mji wa Bunia mashariki mwa Kongo iwapo wapiganaji wote katika eneo hilo hawatasalimisha silaha zao katika muda wa saa 24.
-
Odinga: Sina kinyongo, nimeridhishwa na matokeo ya uchaguzi wa AUC
Feb 15, 2025 23:23Waziri Mkuu wa zamani wa Kenya, Raila Odinga amesema ameridhishwa na mchakato wa uchaguzi wa kumtafuta Mwenyekiti mpya wa Kamisheni ya Umoja wa Afrika (AUC), kurithi mikoba ya Moussa Faki Mahamat.
-
Al-Azhar yawataka Waarabu na Waislamu kupinga kufukuzwa Wapalestina Gaza
Feb 15, 2025 22:55Chuo Kikuu cha Kiislamu cha al-Azhar nchini Misri kimesisitiza kwa mara nyingine tena juu ya kupinga mpango wa kufukuzwa Wapalestina wa Gaza kutoka katika ardhi yao na kuwataka Waarabu na Waislamu kujitokeza na kupinga mpango huo.
-
Kesi 82 za madai ya watu kutoweka nchini Kenya zimeripotiwa tangu Juni 2024
Feb 15, 2025 22:52Nchini Kenya watu wanaituhumu polisi ya nchi hiyo kwa kufanya vitendo vya utekaji nyara lakini bado haijathibitishwa ni nani aliyehusika na utekaji huo.
-
Viongozi wa Umoja wa Afrika wakusanyika kwa mkutano muhimu Ethiopia
Feb 15, 2025 09:04Mkutano wa 38 wa Kawaida wa Umoja wa Afrika umeanza leo Jumamosi katika mji mkuu wa Ethiopia, Addis Ababa, ukiwakutanisha pamoja viongozi wa mataifa kujadili masuala muhimu ya kikanda na bara, ikiwemo amani na usalama, ujumuishaji wa kiuchumi, na mageuzi ya kitaasisi.
-
Guterres aonya kuhusu uwezekano wa vita vya kikanda kutokana na mgororo wa DRC
Feb 15, 2025 08:58Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa, Antonio Guterres, leo Jumamosi amesisitiza umuhimu wa kuheshimu "mipaka" ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo (DRC) na kuepusha vita vya kikanda.
-
Waasi wa M23 waingia Bukavu baada ya kutwaa uwanja wa ndege
Feb 15, 2025 03:42Waasi wa M23 wametangaza habari ya kuingia katika jiji la Bukavu mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
-
Wamorocco wafanya maandamano makubwa ya kuwaunga mkono Wapalestina
Feb 15, 2025 03:39Makumi ya maelfu ya wananchi wa Morocco wamejitokeza katika kona zote za nchi kushiriki maandamano ya kuunga mkono kadhia ya Palestina.