-
Wakenya wapinga sheria za ukaguzi wa magari, wataka zikomeshwe
Jun 29, 2026 12:15Mpango wa serikali ya Kenya wa kulazimisha magari ya kibinafsi kufanyiwa ukaguzi kila mwaka umezua hisia kali miongoni mwa umma, huku waendeshaji magari na viongozi wa upinzani wakitaka ukomeshwe na kuishutumu serikali kwa kuwatwika mzigo mwingine Wakenya wanaopambana na hali ngumu ya maisha.
-
Ripoti ya HRW: Pande zinazopigana Mali zinahusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu
Jun 29, 2026 12:10Pande zinazopigana nchini Mali zinahusika na ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu. Hayo ni kwa mujibu wa ripoti mpya iliyotolewa na shirika la kutetea haki za binadamu la Human Rights Watch (HRW).
-
Wanaharakati waliotoweka Kenya katika maandamano ya Gen Z wapatikana wakiwa wameteswa
Jun 28, 2026 14:07Wanaharakati watano waliotoweka baada ya kukamatwa katika maandamano ya kumbukumbu ya Gen Z ya Juni 25, wamepatikana wakiwa na majeraha na sasa wanapewa matibabu katika Hospitali ya Nairobi Women’s.
-
Mkuu wa Majeshi ya Uganda aamuru kufungwa NTV Uganda na vyombo vingine vya habari
Jun 28, 2026 09:12Mkuu wa Majeshi ya Uganda, Jenerali Muhoozi Kainerugaba ametoa amri ya kufungwa televisheni ya NTV na vyombo vingine vya habari.
-
DRC yaishtaki Rwanda ICJ kwa tuhuma za unyanyasaji
Jun 28, 2026 04:32Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo imewasilisha kesi dhidi ya Rwanda katika Mahakama ya Kimataifa ya Haki ICJ, ikiituhumu nchi hiyo jirani kwa vitendo vya ukatili katika eneo lenye utajiri wa madini la mashariki mwa DRC.
-
Mlipuko wa Ebola waongeza mateso kwa wananchi wa mashariki mwa DRC
Jun 27, 2026 10:55Wajumbe wa Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa wamejulishwa kuwa kuongezeka kwa mapigano, kuzorota kwa hali ya kibinadamu na mlipuko mpya wa Ebola kunazidi kuongeza mateso kwa wananchi wa mashariki mwa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo, (DRC) licha ya juhudi za kikanda za kuleta amani kuendelea kupata mafanikio.
-
Burkina Faso yavunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa, yaituhumu kwa kuingilia mambo yake ya ndani
Jun 27, 2026 10:47Burkina Faso imevunja uhusiano wa kidiplomasia na Ufaransa, na hivyo kuwa taifa jipya zaidi la Afrika Magharibi kujitenga na aliyekuwa mtawala wake wa kikoloni baada ya miaka ya kuzorota kwa mahusiano kati ya pande hizo mbili.
-
Afrika Kusini yaapa kukabiliana vikali na ukatili dhidi ya wahamiaji
Jun 26, 2026 11:10Rais wa Afrika Kusini, Cyril Ramaphosa, ameapa kukabiliana na jaribio lolote la kuyumbisha taifa wakati wa maandamano yaliyopangwa kufanywa wiki ijayo dhidi ya wahamiaji, huku wimbi la chuki dhidi ya wageni lizidi kuongezeka nchini humo.
-
Wafungwa 11 wa kisiasa Tunisia wataka kuanzishwa kambi moja ya upinzani ili kurejesha uhuru
Jun 26, 2026 03:53Wafungwa kumi na mmoja wa Tunisia wameyataka makundi ya upinzani nchini humo "kuungana ili kurejesha uhuru na demokrasia" nchini humo.
-
Polisi yatumia mabomu ya machozi kudhibiti maandamano Kenya
Jun 26, 2026 02:39Polisi nchini Kenya jana walitumia mabomu ya kutoa machozi dhidi ya waandamanaji katika maeneo mbalimbali mjini Nairobi huku makundi yanayoongozwa na vijana yakifanya kumbukumbu ya miaka miwili tangu maandamano ya Gen Z.