-
Hatua mpya ya Baraza la Wawakilishi la Marekani katika kuunga mkono utawala wa Kizayuni
May 19, 2024 07:55Alhamisi Mei 16, Baraza la Wawakilishi la Marekani, Congress, lilikosoa uamuzi wa hivi karibuni wa Rais Joe Biden wa Marekani wa kuzuia kutumwa shehena ya silaha kwa Israel, na kupasisha mswada chini ya anwani "Misaada kwa ajili ya Usalama wa Israel", ambao ulimtaka Biden asizuie tena kutumwa silaha Israeli kwa kisingizio chochote kile.
-
Iran yakanusha taarifa 'isiyokubalika' ya Arab League kuhusu visiwa vyake vitatu vilivyoko Ghuba ya Uajemi
May 18, 2024 23:16Nasser Kan’ani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran, amesisitiza kuwa visiwa vitatu vya Bu Musa na Tunb Kubwa na Ndogo vilivyoko katika Ghuba ya Uajemi vitaendelea kuwa sehemu isiyotenganishika ya ardhi ya Iran na kwamba madai yasiyo na msingi yanayotolewa na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kuhusu suala hilo hayakubaliki kabisa.
-
Onyo la viongozi wa China na Russia kwa Marekani kuhusu Afghanistan
May 18, 2024 03:39Marais Vladimir Putin wa Russia na Xi Jinping wa China wametangaza baada ya mkutano wao huko Beijing kwamba Marekani na NATO zinabeba dhima ya matokeo ya uvamizi wao wa miaka 20 nchini Afghanistan na hazipaswi kujenga miundombinu ya kijeshi katika nchi hiyo.
-
Kuenea vuguvugu la wanafunzi dhidi ya Israel kutoka Chuo Kikuu cha Columbia hadi Oxford
May 18, 2024 00:28Wanachama wa jopo la elimu na wafanyakazi zaidi ya 500 wa Chuo Kikuu cha Oxford nchini Uingereza wameandika barua ya kuunga mkono kambi ya mshikamano na matakwa ya wanafunzi wanaoandamana katika chuo kikuu hicho kuunga mkono Palestina na kulaani jinai zinazofanywa na utawala haramu wa Israel dhidi ya watu wa Gaza.
-
Wazayuni washambulia misafara ya misaada ya kibinadamu huko Gaza
May 17, 2024 05:54Vyombo vya habari vya utawala wa Kizayuni vimeripoti kuwa, walowezi wa Kizayuni wamekuwa wakishambulia malori yanayobeba misaada ya kibinadamu kwa ajili ya watu wa Gaza karibu na mji mtakatifu wa Quds (Jerusalem) katika ardhi zinazokaliwa kwa mabavu.
-
Mafanikio ya uvumbuzi wa wanawake wa Iran katika nyanja mbalimbali
May 17, 2024 03:39Ingawa bado kuna pengo kubwa kati ya wavumbuzi wanawake na wanaume duniani lakini viashiria vilivyopo vinaonyesha kuwa juhudi zinazofanywa na wanawake wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran kwa ajili ya kuziba pengo hilo zinaendelea kwa kasi kubwa.
-
Maandamano ya Wazayuni dhidi ya Baraza la Mawaziri la Netanyahu katika Siku ya Nakba
May 16, 2024 05:47Moja ya matukio muhimu yaliyojiri katika Siku ya Nakba mwaka huu ni maandamano yaliyofanywa na Wazayuni wanaopinga vita dhidi ya Gaza. Wazayuni hao waliandamana mbele ya jengo la Wizara ya Vita ya Israel huko Tel Aviv.
-
Marekani kukanusha tena kutokea mauaji ya kimbari huko Ukanda wa Gaza, ni kukana ukweli ulio wazi
May 16, 2024 00:55Licha ya Wapalestina zaidi ya elfu 35,000 kuuawa shahidi na utawala wa kigaidi wa Israel huko Ukanda wa Gaza, lakini Jake Sullivan, Mshauri wa Usalama wa Taifa wa Ikulu ya White House nchini Marekani amedai bila kuona haya kwamba serikali ya Rais Joe Biden haiyachukulii mauaji hayo kuwa ni mauaji ya halaiki.
-
Sera za Iran kuhusu nishati ya nyuklia hazijabadilika
May 15, 2024 07:21Nasser Kanani, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran alitangaza Jumatatu 13 Mei kwamba, sera za nyuklia za Jamhuri ya Kiislamu ya Iran hazijabadilika.
-
Iran: Haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja
May 14, 2024 23:07Ali Kanani Chafi, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Iran amesema haki za binadamu za Marekani na Israel ni pande mbili za sarafu moja kwani zote zinakiuka pakubwa haki za binadamu dhidi ya mateka na wafungwa, moja huko Negev na nyingine huko Guantanamo na Abu Ghraib.