-
Nukta tano muhimu katika barua ya Islami kwa Grossi kuhusiana na tishio la utawala wa Kizayuni kutumia bomu la nyuklia dhidi ya Ghaza
Nov 11, 2023 07:32Katika barua yake kwa Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA, Mkuu wa Shirika la Nishati ya Atomiki la Iran amelitaka shirika hilo kulibainishia wazi Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa, hatari zinazoweza kusababishwa na matumizi au tishio la matumizi ya silaha za nyuklia za utawala wa Kizayuni dhidi ya wananchi wa Palestina.
-
Kikao cha ECO na sisitizo la kusimamishwa mashambulizi ya Israel Ukanda wa Ghaza
Nov 11, 2023 03:11Waziri Mkuu wa Pakistan, Anwaar-ul-Haq Kakar amesema katika kikao cha wakuu wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiuchumi (ECO) kilichofanyika Tashkent, mji mkuu wa Uzbekistan kwamba, tuna wajibu wa kuziunga mkono juhudi za kukomeshwa mashambilizi na jinai za kivita za utawala wa Kizyauni huko Ukanda wa Ghaza.
-
Mashambulio ya utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza, siku ya 35
Nov 10, 2023 23:58Mashambulio ya utawala wa Kizayuni dhidi ya maeneo ya makazi na miundombinu muhimu huko Ghaza yanaendelea kwa siku ya 36 sasa, ambapo wakazi 30 zaidi wa Ghaza wameuawa shahidi katika shambulio la bomu kwenye nyumba mbili katika kambi ya Jabalia kaskazini mwa Ukanda wa Gaza.
-
Sisitizo la Uturuki la kuendelea kuwepo kijeshi nchini Iraq na Syria
Nov 10, 2023 04:24Mashambulizi ya jeshi la Uturuki dhidi ya Syria na Iraq yamewekwa katika ajenda ya serikali ya Ankara, muda mfupi baada ya Anthony Blinken Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani kufanya safari mjini humo.
-
Utunishaji misuli wa China sambamba na harakati za Marekani katika Bahari ya China Kusini
Nov 09, 2023 23:22China imetuma meli yake ya kivita ya kubeba ndege ya Shangong katika Bahari ya China Kusini sambamba na kufanyika maneva ya baharini kati ya Marekani, Korea Kusini na Ufilipino.
-
Sababu za umuhimu wa kuingia Yemen katika vita vya Gaza
Nov 09, 2023 07:11Katika hali ambayo nchi muhimu za Kiarabu hazijachukua hatua yoyote ya maana mkabala wa jinai za utawala wa Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kujiri maafa ya binadamu katika ukanda huo, serikali ya Uokovu wa Kitaifa ya Yemen yenye makao yake huko Sana'a imetangaza rasmi kuingia vitani dhidi ya utawala wa Kizayuni.
-
Siku ya 33 ya vita vya Gaza: Ubomoaji wa nyumba, hospitali na shule ungali unaendelea
Nov 09, 2023 03:32Kuendelea mashambulizi ya kila upande ya jeshi la Kizayuni dhidi ya Ukanda wa Gaza na kujiri mapigano makali kati ya vikosi vya muqawama na wavamizi hao karibu na kambi ya al-Shati iliyoko magharibi mwa mji wa Gaza, ni baadhi ya habari za hivi karibuni kutoka Palestina inayokaliwa kwa mabavu na utawala ghasibu wa Israel.
-
Netanyahu akataa ombi la Biden la kusitisha mapigano kwa siku 3 huko Gaza
Nov 08, 2023 22:48Rais Joe Biden wa Marekani amemtaka Benjamin Netanyahu Waziri Mkuu wa Israel asitishe mapigano kwa siku tatu ili kutatua suala la mateka. Kuhusiana na jambo hilo, Biden amesema katika mazungumzo ya simu yaliyofanyika siku ya Jumanne alimuomba Benjamin Netanyahu asitishe mapigano ili kuandaa uwanja wa kushughulikiwa suala la mateka wa Israel.
-
Malengo ya utawala wa Kizayuni ya kuainisha muda wa kuondoka raia huko Gaza
Nov 08, 2023 06:59Daniel Hagari, msemaji wa jeshi la utawala wa Israel alitangaza Novemba 6 kuanza usitishwaji vita wa siku mbili kwa ajili ya kutoa fursa kwa wakazi wa kaskazini mwa Ghaza kuondoka katika eneo hilo.
-
Kupunguzwa uhusiano wa kidiplomasia wa Afrika Kusini na utawala wa Kizayuni wa Israel
Nov 08, 2023 03:51Afrika Kusini imetangaza kuwa itawarejesha nyumbani wanadiplomasia wake wote kutoka Israel. Uamuzi huo umechukuliwa kutokana na kuendelea mashambulizi na jinai za Israel dhidi ya watu wa Ukanda wa Gaza huko Palestina.