-
Wasiwasi wa kieneo na kimataifa kuhusu tabia ya ubaguzi wa rangi ya baraza jipya la mawaziri la Israel dhidi ya Wapalestina
Jan 06, 2023 23:07Hatua ya hivi karibuni ya Waziri wa Mambo ya Ndani wa utawala haramu wa Israel, ya kuingia kinyume cha sheria katika Msikiti Mtukufu wa al-Aqsa imekabiliwa na radiamali kali ya kieneo na kimataifa, na ambayo imezipelekea nchi za China na Imarati kuomba kikao cha dharura cha Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa kwa ajili ya kujadiliwa suala hilo.
-
Kuongezeka umaarufu wa Shahidi Haj Qassem Soleimani duniani, hasa barani Asia
Jan 06, 2023 04:20Sambamba na kuadhimishwa mwaka wa tatu wa kuuawa shahidi Luteni Jenerali Haj Qassem Soleimani na Abu Mahdi al-Muhandes, habari na ripoti zilizochapishwa kuhusu kufanyika sherehe katika maeneo mbalimbali duniani zinaonyesha kuwa uungwaji mkono na umaarufu wa jenerali huyo mashuhuri umeongezeka zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma, na hasa miongoni mwa vijana.
-
Kurudi nyuma kwa serikali ya Macron dhidi ya upinzani
Jan 05, 2023 22:50Serikali ya Ufaransa Jumanne wiki hii ilidokeza uwezekano wa kutazamwa umpya mpango tata wa Rais Emmanuel Macron wa kubadilisha sheria za pensheni. Hatua hiyo inaonekana kuwa ni kusalimu amri mbele ya wapinzani wa mpango huo.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu kuhusu dhulma za mfumo wa ubepari wa Magharibi kwa wanawake
Jan 05, 2023 02:01Ubepari wa Magharibi na demokrasia ya kiliberali, ambayo baada ya kuanguka kwa Umoja wa Kisovieti mnamo 1991, kulingana na wanafikra wengine wa Magharibi kama vile Francis Fukuyama, iliushinda mfumo wa kikomunisti kama mfumo bora wa kisiasa na kiuchumi, na kutambuliwa kama mwisho wa historia, sasa unakabiliwa na matatizo makubwa na ya kimsingi.
-
Hisia na misimamo ya nchi za Kiarabu kwa uamuzi wa serikali ya Netanyahu wa kupanua vitongoji haramu vya wazayuni
Jan 04, 2023 23:01Kufuatia uamuzi uliotangazwa na waziri mkuu mpya wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel Benjamin Netanyahu kwamba serikali yake itaendeleza ujenzi haramu wa vitongoji, baadhi ya nchi za Kiarabu zimelaani uamuzi huo na kuipa indhari Tel Aviv kuhusiana na madhara ya hatua hiyo.
-
Kutimuliwa balozi wa Ufaransa Burkina Faso; pigo jengine kwa Paris
Jan 04, 2023 05:32Msemaji wa serikali ya Burkina Faso Jean-Emmanuel Ouedraogo ametangaza kuwa balozi wa Ufaransa Luc Hallade ametakiwa aondoke nchini humo kufuatia kushadidi mgogoro kati ya nchi hizo mbili.
-
Miaka saba tangu kunyongwa Ayatullah Sheikh Nimr Baqi al-Nimr mwanazuoni mtajika wa Saudi Arabia
Jan 03, 2023 22:38Ayatullah Sheikh Nimr Baqi al-Nimr alikuwa mwanazuoni mahiri na mtajika wa eneo la Qatif mashariki mwa Saudi Arabia ambaye kwa kuunga mkono maandamano ya amani ya eneo hilo alikuwa akitaka kukomeshwa ubaguzi dhidi ya Waislamu wa madhehebu ya Shia, na wakati huo huo kufanyike mageuzi katika mfumo wa kisiasa wa nchi hiyo.
-
Luteni Jenerali Qassem Soleimani; nembo ya muqawama na vita dhidi ya ugaidi Asia Magharibi
Jan 03, 2023 04:26Katika kipindi cha miongo kadhaa ya hima na idili, shahidi Luteni Jenerali Qassem Soleimani, alitoa huduma kubwa kwa kambi ya muqawama katika eneo la Asia Magharibi ikiwemo nchini Iraq, Syria, Palestina na Lebanon; huduma ambazo zinmetambuliwa na viongozi wa muqawama kwamba, ni za kudumu na za kubakia milele.
-
Makumi ya Wamarekani, wahanga wa umaskini na baridi kali, huku mabilioni ya dola yakitumiwa kwenye vita vya Ukraine
Jan 02, 2023 22:51Wakati mji wa Buffalo ulioko katika jimbo la New York kaskazini-mashariki mwa Marekani, ukihangaika kujikwamua kwenye athari mbaya za theluji na dhoruba kali, matatizo yaliyosababishwa na maafa hayo makubwa yamedhihirisha zaidi ukosefu wa usawa wa kiuchumi na ubaguzi wa kimbari katika mji huo na Marekani kwa ujumla.
-
Kusajiliwa mauaji ya Kamanda Soleimani katika majukwaa ya kimataifa
Jan 02, 2023 08:21Abbas Ali Kadkhodaei, mkuu wa kamati maalumu ya ufuatiliaji wa kisheria na kimataifa wa mauaji na kuuawa shahidi Kamanda Haj Qassem Soleimani amesema: Mauaji ya Shahidi Soleimani na wenzake yamesajiliwa katika duru za kimataifa kama uhalifu wa kimataifa wa Marekani.