-
Madai yasiyo na msingi ya Pentagon kuhusu sera za kikanda za Iran
Feb 03, 2022 06:41Msemaji wa Wizara ya Ulinzi ya Marekani (Pentagon) amekariri madai yasiyo na msingi kuhusu siasa na sera za Iran katika eneo na kudai kuwa kuna vitisho maalumu kutoka kwa nchi hii.
-
Marekani na Isreal; wachezaji wanaonufaika zaidi na vita vya Yemen
Feb 02, 2022 22:59Akizungumza siku ya Jumanne katika kikao na jumbe mbili za makabila ya eneo la al-Jauf na Maarib ya nchini Yemen, Abdulmalik al-Huthi, Kiongozi cha harakati ya Ansarullah amesema Wamarekai na Waisraeli ni maadui wakuu wa Waislamu na kwamba wanajaribu kunufaika na matatizo yaliyoko katika Umma wa Kiislamu ili kufikia malengo yao haramu katika eneo.
-
Amnesty International: Israel ni utawala wa ubaguzi wa rangi
Feb 02, 2022 08:00Shirika la kutetea haki za binadamu la Amnesty International limeutuhumu utawala wa Kizayuni wa Israel kuwa ni utawala wa baguzi wa rangi wa apartheid. Amnesty Internation inakuwa taasisi ya karibuni zaidi ya kimataifa ya kutetea haki za binadamu kuitangaza Israel kuwa ni utawala wa apartheid.
-
Tarehe 12 Bahman, kumbukumbu ya kurejea Iran Imam Khomeini; kuanza Alfajiri Kumi
Feb 01, 2022 23:03Jumanne ya jana tarehe 12 Bahman kwa mujibu wa kalenda ya Hijria Shamsia iliyosadifiana na tarehe Mosi Februaria 1979 ni siku ya kihistoria ambapo Imam Ruhullah Khomeini muasisi wa Jamhhuri ya Kiisloamu ya Iran alirejea hapa nchini baada ya kuwa uhamishoni kwa miaka 14.
-
Sisitizo la Katibu Mkuu wa UN la kuchungwa haki za msingi za binadamu na Taliban nchini Afghanistan
Feb 01, 2022 00:39Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa amesema, ili serikali ya Taliban nchini Afghanistan iwe na uwanachama katika jamii ya kimataifa na iweze kutambuliwa rasmi, inapaswa kuchunga haki za msingi za binadamu zikiwemo za wanawake.
-
Malengo ya safari ya Rais wa utawala wa Kizayuni wa Israel nchini Imarati
Jan 31, 2022 05:44Isaac Herzog, rais wa utawala haramu wa Kizayuni wa Israel, jana Jumapili tarehe 30 Januari aliwasili mjini Abu Dhabi katika safari ya kwanza rasmi ya kuutembelea Umoja wa Falme za Kiarabu, Imarati.
-
Mtazamo wa Kiongozi Muadhamu; ushindi wa ngome ya uzalishaji katika vita vya kiuchumi vya adui
Jan 31, 2022 00:31Kiongozi Muadhamu wa Mapinduzi ya Kiislamu amesisitiza kuwa, kusimama kidete sekta ya uzalishaji bidhaa za ndani mbele ya hujuma za kiuchumi na njama za adui za kujaribu kuizuia Iran isiuze mafuta na gesi yake, na pia kusimama imara mbele ya vita vya kuifungia Tehran vyanzo vya fedha za kigeni na kupanga njama za kuzuia mabadilishano ya kibiashara ya Iran na nchi nyingine, kwa hakika ni jihadi na ni miongoni mwa ibada kubwa kabisa.
-
Mitazamo tofauti kuhusu sababu za kuondoka wanajeshi wa Imarati huko Ma'arib na Shabwah nchini Yemen
Jan 30, 2022 10:33Viongozi wa Abu Dhabi wametangaza kuwa wameondoa wanajeshi wao katika mikoa ya Shabwah na Ma'rib nchini Yemen, baada ya mashambulio ya kulipiza kisasi na maonyo makali yaliyotolewa na wanamapambano wa Yemen kwa Umoja wa Falme za Kiarabu (Imarati).
-
Takwa la Russia kwa ajili ya kuondoka haraka vikosi vamizi ajinabi huko Syria
Jan 29, 2022 08:46Dmitry Polyanskiy Naibu Mwakilishi wa Russia katika Umoja wa Mataifa amesema katika hotuba yake katika kikao cha Baraza la Usalama la umoja huo kuwa Russia inataka kuondoka haraka iwezekanavyo vikosi vyote vamizi ajinabi ambavyo vipo kinyume cha sheria huko Syria.
-
Kuendelea mgogoro wa kisiasa dhidi ya waziri mkuu wa Uingereza
Jan 28, 2022 23:26Kufuatia kufichiliwa habari ya uwezekano wa ofisi ya waziri mkuu wa Uingereza kuvunja kanuni na sheria za corona, polisi ya nchi hiyo imeanzisha uchunguzi wa kubaini ukweli wa jambo hilo.