-
Kupasishwa azimio jipya la Umoja wa Mataifa la kuwaunga mkono Wapalestina
Nov 16, 2024 08:30Kamati ya Haki za Binadamu na Masuala ya Kibinadamu ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa imepasisha azimio na kusisitiza kuwa wananchi wa Palestina wana haki ya kujiainishia mustakbali wao katika ardhi za Palestina, na kwamba wana haki ya kuwa huru, kujitawala na kujikomboa haraka kutoka katika makucha ya ukaliaji mabavu wa utawala wa Kizayuni.
-
Juhudi za Marekani za kuhalalisha jinai za Israel na kuendelea kuitumia silaha za mauaji ya umati
Nov 15, 2024 23:20Vedant Patel, Msemaji wa Wizara ya Mambo ya Nje ya Marekani, ametoa matamshi ambayo yanaonyesha kuwa Marekani haiko tayari kwa vyo vyote vile kumuwajibisha mshirika wake wa jinai za kivita, yaani utawala haramu wa Israel, na kuwa inatosheka tu kwa kutoa madai matupu yasiyo na maana kuhusiana na suala zima la haki za binadamu.
-
Njama mpya ya Israel ya unyakuzi wa ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan
Nov 15, 2024 05:52Bezalel Smotrich, Waziri wa Fedha wa utawala wa Kizayuni ametoa matamshi kuhusiana na ushindi wa Donald Trump katika uchaguzi wa rais wa Marekani na kusema kuwa, mwaka 2025 utakuwa mwaka wa utawala huo ghasibu kunyakua na kupanua udhibiti wake katika ardhi ya Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan.
-
Safari ya Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki nchini Iran
Nov 14, 2024 08:44Rafael Grossi, Mkurugenzi Mkuu wa Wakala wa Kimataifa wa Nishati ya Atomiki IAEA aliwasili mjini Tehran Jumanne jioni ambapo amekutana na kuzungumza na viongozi husika wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran.
-
Iran yaionya Marekani kuhusu kukariri siasa zilizofeli za mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa
Nov 14, 2024 06:04Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran ameionya Marekani dhidi ya kuanzisha tena kampeni yake ya "mashinikizo ya kiwango cha juu kabisa" dhidi ya Tehran na kusisitiza kwamba, majaribio ya hapo awali ya Washington ya kuishinikiza Iran yalishindwa na kugonga mwamba.
-
Msimamo mmoja wa nchi za Kiislamu na Kiarabu katika kulaani jinai za Israel dhidi ya Gaza
Nov 13, 2024 23:09Kikao cha dharura cha viongozi wa nchi wanachama wa Jumuiya ya Ushirikiano wa Kiislamu na Jumuiya ya Nchi za Kiarabu kwa ajili ya kuunga mkono kadhia ya Palestina kilifanyika siku ya Jumatatu mjini Riyadh Saudi Arabia, ambapo msimamo wa pamoja unaolaani jinai za kinyama za utawala wa Kizayuni dhidi ya watu wa Palestina Lebanon ulipitishwa katika taarifa ya mwisho ya kikao hicho.
-
Kuimarishwa uhusiano wa kiusalama kati ya Iran na Pakistan
Nov 13, 2024 04:17Sayyid Abbas Araghchi, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa Jamhuri ya Kiislamu ya Iran, amesema kuwa katika safari yake ya hivi karibuni nchini Pakistan, ameshauriana na viongozi wa kijeshi na kisiasa wa nchi hiyo kuhusiana na namna ya kukabiliana na ugaidi, ambayo ni changamoto kubwa zaidi katika eneo.
-
Matukio ya Amsterdam dhihirisho la utambulisho halisi wa Wazayuni
Nov 12, 2024 22:45Kinyume na riwaya na simulizi iliyogeuzwa ya ghasia za Wazayuni huko Amsterdam Uholanzi, sasa Wazayuni wavamizi katika nchi nyingine za Ulaya pia wanahisi kutokuwa na usalama.
-
Azma ya Iran na Saudi Arabia ya kuimarisha uhusiano baina yao
Nov 12, 2024 06:49Viongozi wa ngazi ya juu wa majeshi ya Iran na Saudi Arabia wamejadili njia za kuboresha diplomasia ya ulinzi kati ya nchi mbili huku utawala wa Kizayuni wa Israel ukiendelea kuzidisha mivutano na wasiwasi katika eneo la Magharibi mwa Asia.
-
Kushadidi hitilafu katika Umoja wa Ulaya
Nov 12, 2024 00:24Katika miaka ya hivi karibuni, nchi wanachama wa Umoja wa Ulaya zimekuwa zikikabiliwa na mizozo kuhusu masuala mbalimbali ya kisiasa na kiuchumi, mizozo ambayo imezidi kuongezeka kutokana na kuendelea vita vya Russia na Ukraine, hivi kwamba sasa vita hivyo vimekuwa miongoni mwa migogoro mikuu zaidi katika umoja huo.