Kukiri Israel juu ya kutekeleza ufutaji kizazi katika Ukanda wa Gaza
https://parstoday.ir/sw/news/west_asia-i119668-kukiri_israel_juu_ya_kutekeleza_ufutaji_kizazi_katika_ukanda_wa_gaza
Waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel Moshe Yaalon amesisitiza kwa mara nyingiine tena kwamba, utawala huo unafanya "maangamizi ya kizazi" kaskazini ya Ukanda wa Gaza, akimshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kuielekeza Israel kwenye "uharibifu."
(last modified 2024-12-03T23:15:20+00:00 )
Dec 03, 2024 23:15 UTC
  • Kukiri Israel juu ya kutekeleza ufutaji kizazi katika Ukanda wa Gaza

Waziri wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni wa Israel Moshe Yaalon amesisitiza kwa mara nyingiine tena kwamba, utawala huo unafanya "maangamizi ya kizazi" kaskazini ya Ukanda wa Gaza, akimshutumu Waziri Mkuu Benjamin Netanyahu kwa kuielekeza Israel kwenye "uharibifu."

Akizungumza katika mahojiano na idhaa ya Israel ya Democratv, Yaalon ambaye amewahi pia kuwa mkuu wa jeshi la Isreal amekosoa sera inazotekeleza serikali ya mrengo wa kulia ya Netanyahu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan na Gaza na akasema: "tunaburutwa kupelekwa kwenye uvamizi, unyakuzi wa ardhi, maangamizi ya kizazi - tazama kaskazini mwa Gaza— uhamishaji na ujengaji wa vitongoji vya Wayahudi.”

Yaalon, ambaye aliwahi kuwa waziri wa vita wa utawala wa Kizayuni kuanzia 2013 hadi 2016, amesisitiza katika mahojiano hayo kwamba, vitendo vinavyofanywa na jeshi la Israel katika eneo la Gaza la Palestina ni sawa na "maangamizi ya kizazi".

Mtangazaji aliyemhoji alimkatiza wakati anaeleza hayo na kumuuliza: “nimekusikia kwa usahihi? Ni maangamizi ya kizazi kaskazini mwa Gaza—unadhani tunaelekea kwenye njia hiyo?” Yaalon akajibu: “Kwa nini useme tunaelekea ‘kwenye njia’? Kwani nini kinatokea huko? Beit Lahia haipo tena, Beit Hanoon haipo tena, na sasa wanaifanyia kazi Jabalia. Wao (jeshi la Israel) wanalifuta eneo la Waarabu."

Vitongoji haramu vya walowezi wa Kiyahudi

 

Kwa hakika Israel ni misdaqi na mfano wa wazi wa utawala wa kibaguzi (apartheid) duniani. Utawala huu ulioasisiwa chini ya kivuli cha sera za kikoloni za Waingereza na kukalia kwa mabavu ardhi ya Palestina mwaka 1948, umetekeleza ubaguzi wa rangi dhidi ya Wapalestina kwa kipindi cha miaka 76 iliyopita. Mauaji dhidi ya watu wasio na hatia na unyakuzi wa ardhi ya wananchi wa Palestina ni sehemu ya utambulisho wa utawala wa Kizayuni kuanzia wakati huo hadi leo.

Kwa kujenga vitongoji vya walowezi wa Kiyahudi, utawala huo ghasibu pia umebadilisha sura na muundo wa wakazi wa ardhi za Palestina.

Takwimu zinaonyesha kuwa, mwaka 1948 Wapalestina walikuwa wakimiliki asilimia 94 ya ardhi ya nchi yao ya Palestina, huku Wazayuni waliokuwa wakitumia "ghilba na nguvu" wakimiliki asilimia 6 tu ya ardhi hiyo; lakini siasa za kujipanua za Wazayuni zimesababisha hali hiyo sasa kuwa kinyume chake.

Ukweli wa mambo ni kuwa, utawala wa Telv Aviv unafanya kila njia kubadilisha mlingano wa idadi ya watu katika Ukingo wa Magharibi wa Mto Jordan ili idadi ya Wapalestina izidi kupungua na ile ya Mayahudi iongezeke zaidi.

Pamoja na hayo yote, yaliyowapata Wapalestina katika kipindi cha miezi 13 iliyopita kutokana na vita vya Gaza ni jambo ambalo kimsingi halina mithili wala mfano. Takriban Wapalestina 50,000 wameuawa shahidi, zaidi ya watu 100,000 walijeruhiwa na zaidi ya watu milioni 2 wamekimbia makazi yao tangu Israel ilipoanzisha hujuma na mashambulio ya kinyama hukko Gaza Oktoba mwaka jana (2023).

Hapana shaka kuwa, jinai hizo ni mfano wa wazi wa ufutaji kizazi unaofanywa na Israel huko Gaza, kiasi kwamba kwa mara ya kwanza baadhi ya maafisa wa zamani wa utawala huo kama Moshe Ya'alon na vyombo vya habari vya Kiebrania kama vile "Haaretz" wanakiri dhahiri na bayana kwamba utawala wa Kizayuni unatafuatilia kuhamishwa kwa nguvu wakazi wa Gaza na kufanywa mauaji ya kimbari dhidi ya wakazi wa Ukanda huo ambao ni ngome imara ya muqawama wa Palestina.

Karibu Wapalestina 50,000 wameuawa shahidi tangu utawala haramu wa Israel ulipoanziisha hujuma na mashambulio ya kinyama dhidi ya Gaza

 

Kukiri waziri huyo wa zamani wa vita wa utawala wa Kizayuni kulikuwa na uchungu mkubwa kwa baraza la mawaziri la Netanyahu kiasi kwamba, baadhi ya mawaziri wamekosoa vikali kauli ya Ya'alon na kuieleza kuwa ni ya kubuni kichwani na ya kuudhi, jambo ambalo litatoa pigo kubwa kwa kile waliichokitaja kuwa 'haiba na hadhi ya Israel' kieneo na kimataifa.

Akijibu matamshi hayo ya Moshe Ya'alon, Itamar Ben-Gvir, Waziri wa Usalama wa Ndani wa utawala wa Kizayuni wa Israel amesema: "matamshi haya kuhusu mauaji ya kimbari huko Gaza ni ya uwongo, ya kubuni kichwani, hatari, na yanachafua sura ya Israel duniani."

Akijibu maneno ya Ya'alon, Waziri wa Mashauri ya Kigeni wa wa utawala huo, Gideon Sa;ar, amesema, "matamashi  ya Moshe Ya'alon ni ya kuchukiza na yatatuletea madhara, ulimwengu wa Kiarabu unakariri maeno yake, lakini hakuna uthibitisho wa hili."

Licha ya makemeo na ukosoaji huo, Ya'alon alikariri: "Sitarudi nyuma, Israel inatekeleza mauaji ya kizazi katika Ukanda wa Gaza, kubomoa nyumba za wakaazi wake na kuwafukuza ili kujenga makazi ya Wayahudi.

Hatua ya asasi za kimataifa pia inathibitisha kauli ya Ya'alon kuhusu ufutaji wa kizazi huko Gaza. Hivi karibuni, Mahakama ya Kimataifa ya Jinai (ICC) sanjari na kuulaani utawala wa Kizayuni kwa kufanya jinai za kivita huko Gaza, ilitoa waranti wa kukamatwa Benjamin Netanyahu, Waziri Mkuu na Yoav Gallant, Waziri wa Vita wa utawala huo aliyefukuzwa kazi.

Uamuzi wa Mahakama ya ICC umepongezwa na kukaribishwa kwa mikono miwili kote duniani na nchi nyingi zimetangaza kwamba, zikko tayari kutekeleza uamuzi huo na kuwakamata Netanyahu na Gallant ikiwa watafanya safari katika nchi hizo.