UNRWA: Zaidi ya watoto 540 wameuawa shahidi huko Gaza kila mwezi
Aug 20, 2025 08:02 UTC
Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) limetangaza kuwa: Katika kipindi cha miezi mitano iliyopita, zaidi ya watoto 540 wameuawa shahidi katika mashambulizi ya jeshi la utawala wa Kizayuni katika Ukanda wa Gaza.
Shirika la Misaada na Ajira kwa Wakimbizi wa Kipalestina (UNRWA) liliongeza Jumanne kwamba: Takwimu hii ya kushangaza inaonyesha ukubwa wa maafa ambayo watoto wa Kipalestina wanakabiliwa nayo katika Ukanda wa Gaza. Kwa mujibu wa ripoti hii, hali ya maisha huko Gaza imekuwa mbaya sana kutokana na kuendelea mashambulizi na ukosefu wa chakula, dawa na maji ya kunywa.